DART yaendelea kupiga kalenda usafiri wa Mwendo kasi Mbagala

Joined
Jun 26, 2024
Posts
33
Reaction score
46
Huduma ya mabasi ya mwendokasi iliyotarajiwa kuanza leo Septemba Mosi, 2025 katika barabara ya Mbagala, imesogezwa mbele ikiwa ni sababu ya kutokamilika kwa miundombinu muhimu kama mageti janja na kituo cha kujazia gesi.

Akizungumza lna gazeti la Mwananchi leo Jumatatu, Septemba mosi 2025 , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Dk Athuman Kihamia, amesema kuchelewa kuanza kwa huduma hiyo kunatokana na changamoto hizo, licha ya mabasi kuwa tayari yamewasili. "Mageti janja kwa ajili ya ukataji wa tiketi bado hayajafungwa na kituo cha kujazia gesi kilichopo kwenye karakana ya Mbagala nacho hakijakamilika" alisema Dk. Kihamia.

Ameahidi kutoa taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya ujenzi huo tutaitoa baada ya wiki moja kutokea leo.

Ikumbukwe Mabasi hayo 151 yaliwasili katika karakana ya Mbagala Rangi Tatu tangu usiku wa Agosti 29, 2025.

Je wakati wanaahidi kuanza safari hizo siku ya leo Septemba Mosi, 2025 hawakua na taarifa kamili za maendeleo ya miundo mbinu hiyo, ndio wameshtukizwa leo???

1756722049372.png

1756722101617.png
 
Ni nchi ya hovyo tu, isiyozingatia umakini kwa namna inavyofanya mambo yake.

The way individuals tupo irresponsible katika kuendesha familia zetu, hata wanaoongoza nchi wapo wapo tu.

Africans tuna matatizo makubwa sana...
 
hahaha Kwanini jiji jipya la Dodoma hawa kuweka njia za mwendo kasi?

wao wana mtandao wanasema watanzania tuna kipaji cha ujinga, ngoja wapige pesa.
 
Aliyenunuliwa haya mabasi anayeitwa Mwekezaji bado hajafika, yaani barabara zetu na magari ni yetu halafu yeye anakuja kukusanya tu hela!

Poor Tanzania!
 
Huduma ya mabasi ya mwendokasi iliyotarajiwa kuanza leo Septemba Mosi, 2025 katika barabara ya Mbagala, imesogezwa mbele ikiwa ni sababu ya kutokamilika kwa miundombinu muhimu kama mageti janja na kituo cha kujazia gesi.

Akizungumza lna gazeti la Mwananchi leo Jumatatu, Septemba mosi 2025 , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Dk Athuman Kihamia, amesema kuchelewa kuanza kwa huduma hiyo kunatokana na changamoto hizo, licha ya mabasi kuwa tayari yamewasili. "Mageti janja kwa ajili ya ukataji wa tiketi bado hayajafungwa na kituo cha kujazia gesi kilichopo kwenye karakana ya Mbagala nacho hakijakamilika" alisema Dk. Kihamia.

Ameahidi kutoa taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya ujenzi huo tutaitoa baada ya wiki moja kutokea leo.

Ikumbukwe Mabasi hayo 151 yaliwasili katika karakana ya Mbagala Rangi Tatu tangu usiku wa Agosti 29, 2025.

Je wakati wanaahidi kuanza safari hizo siku ya leo Septemba Mosi, 2025 hawakua na taarifa kamili za maendeleo ya miundo mbinu hiyo, ndio wameshtukizwa leo???

View attachment 3461130

View attachment 3461132
Imesogezwa mbele ili afanyie kampeni mgombea wa CCM atakapokwenda Mbagala.
 
NCHI NGUMU SANA hii, hivyo Wakati Mwekezaji Kaagiza hayo Mabasi Mapema, Hawa Watu Waliokuwa Wanasimamia ujenzi wa hiyo Miundombinu Walikuwa WAPI? Si Wakisema Miundombinu yote Imemalizika, Why Leo Tunasikia Mageti Janja Bado + KITUO Cha kujazia Gesi Nacho Bado? NCHI NGUMU SANA hii
 
Huduma ya mabasi ya mwendokasi iliyotarajiwa kuanza leo Septemba Mosi, 2025 katika barabara ya Mbagala, imesogezwa mbele ikiwa ni sababu ya kutokamilika kwa miundombinu muhimu kama mageti janja na kituo cha kujazia gesi.

Akizungumza lna gazeti la Mwananchi leo Jumatatu, Septemba mosi 2025 , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Dk Athuman Kihamia, amesema kuchelewa kuanza kwa huduma hiyo kunatokana na changamoto hizo, licha ya mabasi kuwa tayari yamewasili. "Mageti janja kwa ajili ya ukataji wa tiketi bado hayajafungwa na kituo cha kujazia gesi kilichopo kwenye karakana ya Mbagala nacho hakijakamilika" alisema Dk. Kihamia.

Ameahidi kutoa taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya ujenzi huo tutaitoa baada ya wiki moja kutokea leo.

Ikumbukwe Mabasi hayo 151 yaliwasili katika karakana ya Mbagala Rangi Tatu tangu usiku wa Agosti 29, 2025.

Je wakati wanaahidi kuanza safari hizo siku ya leo Septemba Mosi, 2025 hawakua na taarifa kamili za maendeleo ya miundo mbinu hiyo, ndio wameshtukizwa leo???

View attachment 3461130

View attachment 3461132
Changamoto hutokea tu ni sehemu ya maisha,tuwe wavumilivu tuwape muda kidogo
 
Hii ndio Tanganyika ya wanyonge wasio n haki.
 
Watumie sasa huu muda kuhakikisha pikipiki haziingii kwenye njia ya mwendo kasi,

Zile taa za barabarani trafiki wahakikishe zinatumika na kufuatwa, kwa sababu itakuw ujinga na udhihirisho wa kwamba kila sekta tunapigwa,

Haiwezekani wingi wa taa zile alafu hazifitwi kama hazitotumika walioziweka wachukue taa na kurudisha hela za wananchi
 
Huduma ya mabasi ya mwendokasi iliyotarajiwa kuanza leo Septemba Mosi, 2025 katika barabara ya Mbagala, imesogezwa mbele ikiwa ni sababu ya kutokamilika kwa miundombinu muhimu kama mageti janja na kituo cha kujazia gesi.

Akizungumza lna gazeti la Mwananchi leo Jumatatu, Septemba mosi 2025 , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Dk Athuman Kihamia, amesema kuchelewa kuanza kwa huduma hiyo kunatokana na changamoto hizo, licha ya mabasi kuwa tayari yamewasili. "Mageti janja kwa ajili ya ukataji wa tiketi bado hayajafungwa na kituo cha kujazia gesi kilichopo kwenye karakana ya Mbagala nacho hakijakamilika" alisema Dk. Kihamia.

Ameahidi kutoa taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya ujenzi huo tutaitoa baada ya wiki moja kutokea leo.

Ikumbukwe Mabasi hayo 151 yaliwasili katika karakana ya Mbagala Rangi Tatu tangu usiku wa Agosti 29, 2025.

Je wakati wanaahidi kuanza safari hizo siku ya leo Septemba Mosi, 2025 hawakua na taarifa kamili za maendeleo ya miundo mbinu hiyo, ndio wameshtukizwa leo???

View attachment 3461130

View attachment 3461132
There is no hurry in africa
 
Back
Top Bottom