Dark days 17/03/20

Mawazo mazuri isipokuwa 35
 
Ni vizuri kuliombea taifa letu kwenye vipindi vya shida na raha, hususan kwenye vipindi ambavyo kuna political tensions na rumours za mipango ya maandamano.

Unaweza ukaisambaza sala hii hapo chini kwenye makundi ya whatsapp.


Sala ya kuliombea taifa letu la Tanzania, Tanganyika, Unguja na Pemba.


Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.

Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.

Utupe leo mkate wetu wa kila siku.

Utusamehe makosa yetu, kama tunavyo wasamehe na sisi waliotukosea.

Usitutie katika kishawishi, lakini utuokoe kutoka maovuni.

Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele, Amen.

Eee Adonai YAHWEH El wa Abraham, Isaac na Jacob, muumba wa mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo, tunaomba ulisaidie, ulitajirishe na ulistawishe sana, taifa letu la Tanzania, Tanganyika, Unguja na Pemba, na watu wake, na ulipe (na uwape watu wake) afya nzuri sana, amani, furaha, ustawi, utajiri mwingi sana, haki, katiba nzuri sana, serikali nzuri sana, sera nzuri sana, maisha marefu sana, uzima tele na uzima wa milele. Na pia ulisaidie na uwasaidie watu wake na makabila yake katika mambo yao yote mazuri na kwenye mahitaji yao yote mazuri na kwenye shida zao zote halali, na pia uwasaidie wapendane. Na pia ulikinge na uwakinge watu wake wasipate misukosuko ya kisiasa na ya kijamii. Na pia uli inue liwe taifa bora na la mfano mzuri barani Afrika.

Na pia ulisaidie lisionewe na taifa lolote wala lisionee taifa lolote.

Na pia ulisaidie li ipende injili ya kweli ya Mwanao Yahushua Mashiach.

Tunaomba utusaidie kwenye matatizo yetu yote tunayo yajua na tusiyo yajua. Na pia tuna yaombea mataifa mengine na makabila mengine ya Afrika na duniani.

Tunaomba haya yote ee Adonai YAHWEH El wa Abraham, Isaac na Jacob na tunakushukuru kwa mema yote uliyotufanyia kwa kupitia damu ya Mwanao Yahushua Mashiach iliyomwagika msalabani, na kwa kupitia neema, rehema, huruma na jina la Mwanao Yahushua Mashiach, Bwana na Mwokozi wetu, Amen. Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, Amen.

Sala imeishia hapo.

Siku ya saba ya kibiblia (sabato) ina anza jua linapozama Ijumaa (Friday), na kuisha jua linapozama Jumamosi (Saturday).

Wakristo kutoka mataifa (uncircumcised gentiles christians), kwa neema ya Bwana Yesu Kristo, hawakutakiwa kuishika sabato ya siku ya saba (Matendo ya mitume sura ya 15, na sura ya 19: 20-25). Kama wanataka, wanaweza kusali au na kufanya ibada siku hiyo, na baada ya hapo kuendelea na shughuli zao za kawaida za kidunia.

Kama wanataka wanaweza kusali au na kufanya ibada siku yoyote ya wiki, including siku ya kwanza ya wiki (Jumapili), na baada ya hapo kuendelea na shughuli zao za kawaida za kidunia.

Ila siku ya kwanza ya wiki sio sabato, na pia siku ya kwanza ya wiki sio siku ya Bwana, ingawa Bwana Yesu Kristo alifufuka siku hiyo. Note that siku zote za wiki ni za Bwana, na siku ya saba ndio specifically siku yake.

Wakristo wote wayahudi na mataifa (jews and gentiles christians), wataishika sabato ya siku ya saba, kila wiki, wakiwa mbinguni kwa miaka 1,000, miaka hiyo 1,000, kwa ujumla wake, pia ni sabato ya miaka 1,000 mbinguni.

Pia wakristo wote (jews and gentiles christians), wataishika sabato ya siku ya saba, kila wiki, milele yote, wakiwa Yerusalemu mpya, kwenye dunia mpya na mbingu mpya. Pia milele yote hiyo, kwa ujumla wake, ni sabato ya milele.


Palmoni - The Wonderful Numberer, The Numberer of Secrets
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…