Darasa la saba

Nov 2, 2020
68
90
Wakuu hamjambo,

Vijana wetu wa darasa la Saba wako mtaani kwa muda wa miezi mitatu Hadi hapo watakapojiunga na kidato cha kwanza mwezi Januari mwakani.

Kwa umuhimu wa kipindi hiki na ukizingatia wengi wanatoka shule za msingi za serikali ni muda sasa kwa wahitimu wa kada ya ualimu na nyinginezo, kujitoa kulisaidia kundi hili.

Kwa uzoefu wadogo zetu wanahitaji maarifa mepesi yatajayowapa mwanga wa wanapaswa kujifunza sekondari.

Lugha ya kiingereza ina nafasi kubwa kama msingi wa lugha ya ufundishaji wanafunzi kwa kiwango walichopo.

Unaweza anza na wachache ulio jirani nao, na kwa gharama ya kawaida tu ambayo inalenga kutoa msaada kwao.

Kwa moyo wa aina hii Hadi Januari kufika,Hakika watakua wamepiga hatua kubwa katika maisha yao ya kitaaluma.

Youth Worker

Hardness,Teaches
 
Back
Top Bottom