Darasa la kupigilia pamba kijanja

Jackline Aloyce

Senior Member
Joined
Aug 31, 2016
Messages
112
Points
225

Jackline Aloyce

Senior Member
Joined Aug 31, 2016
112 225
Habari wakuu,

Nimeona na mimi nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu katika maisha.

1.Epuka kuvaa marangirangi
Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza idadi ya rangi,rangi 3 tu zinatosha kukutoa bomba.


2. Vaa kulingana na mazingira/sehemu
Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na mazingira,sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la Wazza kwenye sherehe


3. Masharti ya kuchomekea;
* Marufuku kuvaa oversize/undersize
* Usivae mlegezo
* Hakikisha singlet haionekani
* Usivae mkanda mrefu
* Usivae makubanzi/sandals
* Hakikisha umemach rangi


4. Kama umevaa pensi /kaptula...
* Hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana
* Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi
* Haipendezi kuchemekea
* Hakikisha miguu ni soft


5. Usivae shati jeupe kama la mwanafunzi
Shati nyeupe ni nzuri kama unaijulia wakati unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote ile au ni ya kimtindo sio kuvaa shati la shule.


6. Hakikisha una suruali nyeusi
Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch mashati ya rangi nyingi.


7. Saa
*Kama umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa saa ya aina yoyote
*km umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka kuvaa saa ya mkanda wa plastic.


8. Miwani
Duh hapa pagumu kidogo lakini cha msingi zingatia muundo wa kichwa chako pamoja na aina ya macho uliyonayo na aina ya pamba ulizovaa pia.Sio umepiga jeans kali,kichwa kama madenge na macho kama bundi kisha unapiga miwani ndogo ya njano,ni kituko


9/.Vaa kofia za kijanja
Kofia pia huongeza mvuto,chagua kofia kulingana na aina ya kichwa na mavazi uliyovaa,haipendezi kuvaa suti na kapelo.Kanzu sharti ivaliwe na barakashia ndo utaeleweka la sivyo ni sawa na kuvaa dera tu


10/Mkanda
*Usivae mkanda mrefu km vile umefunga nyoka kiunoni
*Mikanda ya vitambaa au madoidoi inafaa kuvaliwa na jeans/kadeti/kaptula
*Jitahidi mkumatch rangi ya mkanda na viatu kama umevaa nguo za kuchomekea
*Zingatia upana wamkanda na rux za nguo yako


11/ Tupia cheni za ukweli
Mikufu ya kiume pia huongeza mvuto
* Kama umevaa nguo za kuchomekea au suti itapendeza ukivaa cheni ndogo ambayo haitokezi nje ya shati
*Kama umepiga pamba za kishua mfano T.shirt na jeans hapa tupia cheni kubwa lakini hata cheni ndogo zinakubali


12/Uvaaji wa Tie
*Vaa kulingana na urefu wako
*Km wewe mwembamba inapendeza kuvaa tie nyembamba
*Jitahidi kumatch tie na rangi ya shirt/suruali
*Hakikisha tie yako imefungwa vizuri shingoni


13/T.shirt na Jeans
Wanaume wajanja wa mjini hupenda kupiga t shirt na jeans na chini kutupia raba Kali.....Vazi hili lina mvuto wa aina yake hasa limivaliwa kitaani na sehemu za mitoko km vile kwenye Club za starehe


14/Vaa viatu kijanja
Hapa pia Kuna changamoto
*Usivaa suruali ya kitambaa na Raba
*Usivae suruali ya kuchomekea na makubanzi
*Ukipiga jeans unaweza kumatch t.shirt/shirt na rangi ya viatu
*Ukivaa suti yakupasa upige kiatu kikali ....ulikosea itakuwa sawa na Toyota Mark X yenye matairi ya Fuso !!!***Usipojua kuvaa utadharaurika***

The Bitoz
Waoh na kwa wadada utoe maana
 

Forum statistics

Threads 1,380,729
Members 525,856
Posts 33,777,932
Top