Darasa kwa Kubenea na Wabunge wengine

Darasa kwa Kubenea na Wabunge wengine

Tuna mihimili mikuu mitatu kiuongozi kwa mujibu wa Katiba ya JMT. Utawala, Mahakama na Bunge.

Muh. Rais ndiye kiongozi mkuu wa utawala. Vilevile ndiye msimamizi mkuu wa mahakama na bunge. Jaji mkuu na Spika wako chini yake. Kimkoa na kiwilaya, Rais anawakilishwa na Wakuu wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya.

Wakuu Wa wilaya, wakuu Wa mikoa hata ulaya na marekani wapo. Japo majina (title) yanatofautiana, lkn majukumu yao ni kumuwakilisha rais. wabunge kote duniani siyo viongozi Wa kiutendaji (executive).

Nchi zote zina executive, judiciary na legislature. Katika kila nchi executive (Rais na wasaidizi wake) ndiyo watekelezaji Wa sheria kiuongozi. Marekani magavana (tuwaite wakuu Wa mikoa na wilaya) wana nguvu sana kiutendaji.

Licha ya Kubenea kuwa mbunge alipaswa kumheshimu Mkuu Wa wilaya Bila kubishana nae hadharani au kumtukana. Alimuita mhuni na kibaka hadharani.

Makonda ili kuhifadhi ushahidi, aliamua kuteka video camera ya star TV ili ushahidi Wa matusi aliotukanwa usifutwe.

Jiweke katika nafasi ya Makonda. Rais Wa wilaya kutukanwa hadharani. Ikumbukwe kuwa Makonda alikua ameahidi kumpeleka waziri kiwandani Leo.

Kiprotokali baada ya Makonda kuongea na wafanyakazi, Kubenea hakua na haki ya kutaka kuongea baada ya DC. DC aliogopa kuwa maneno ya Kubenea yanaweza chafua hali ya hewa ambayo ilikua imetulia.

Makonda kwa nafasi yake ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika wilaya anayoiongoza. Pangetokea vifo pale kiwandani angelaumiwa Mkuu Wa wilaya. Kubenea anapaswa kulijua hili.

Tabia ya kijeuri ya Kubenea aliionesha siku ya kufungua bunge alipomuomba Kange Lugola kufuta maneno yake. Alitumia lugha ya kibabe sana bila ulazima. Siku hiyo ndiyo nilibaini kuwa Kubenea ana uwezo mdogo wa kujenga hoja. Ni nadra kwake kutumia busara na hekima. Kubenea ajue kuwa kinga anayo bungeni (legislature) siyo uraiani (executive) kwa akina Makonda.

Kubenea alikua na dhamira ya kuwatetea wafanyakazi Wa kiwanda lakini njia aliyoitumia ya jazba na ubabe haikuwa sahihi. Mwl Nyerere aliwahi kuwaambia wanafunzi Wa UDSM walioandamana kuwa "The objectives you have are genuine but the methods you used to achieve your objectives are improper, thus, tarnishing everything".

Tuweke siasa kando. Tuseme ukweli. Katiba ya 1977 ndiyo ituongoze hata kama INA mapungufu. Sheria ni msumeno.

Naamini ya kuwa umeandika kwa kuchukua msimamo wa kati na kati,hukuegemea upande wowote na umejitahidi kuweka hoja nzito kwa kile unachokiamini,hongera.
Binafsi ningependa kuongea na Kubenea nikiamini ya kuwa Kubenea ni mhanga wa vitendo vya dola.Kumwagiwa tindikali kulihisishwa na makala zake katika gazeti la Mwanahalisi.
Napenda kumjulisha Kubenea kuwa pamoja na mateso yote ya gerezani Mandela hakuingia kwenye U Rais na chuki ila mshikamano na watu wake wote.
Kwa mnaasaba huo namuomba Kubenea afiche anachoamini kuhusu dola na anze upya kama mbunge,awe tayari kushirkiana na viongozi wa serikali hata kama anaamini ya kuwa ndo waliomwagia tindikali.
"Hasira ni kama tindikali ,inaharibu chombo ilichohifadhiwa kuliko kule ilikodhamiriwa kumwagwa"
Huchachelewa Kubenea!!!!!!!!!!
 
Mleta mada kupitia reference ya uongozi wa USA umepotosha sijui ni makusudi au hajui?. Na kama hujui iweje uzungumzie kitu usicho kijua kwa mtindo wa kuelekeza /kufundisha?

Kwa upande wangu DC Makonda inabidi akubali kushirikiana na mbunge hata kama wanatofautiana itakadi ya vyama.

Kwanini alikuwa hataki MP Kubenea asizungumze na wapiga kura wake?. Anabidi haeshimu maamuzi ya wananchi walio mchagua huyo MP sizani kama angekuwa Masaburi ndio MP angemyima nafasi ya kuzungumza?

Kingine Makonda aache kukurupuka hana busara hata kidogo then anazani yeye ndio kila kitu.. Atapata shida katika utendaji wake maana ana amini yeye kama yeye anaweza kustand alone kiutekezaji.
 
bunge na mahakama zipo chini ya rais??? umelogwa wewe. bunge, serikali, na mahakama ni taasi ambazo hakuna iliyo juu wala chini ya nyingine. nyambafu!
 
Sijaandika hivyo. Kasome tens uzi wangu

Simpendi Makonda lakini ulichoandika ni very right
Kubenea naona bado sana kisiasa..ana mihemko na kutaka
kuonekana yupo serious kuliko hali halisi..

Makonda hafai lakini sheria zinamlinda
 
Nashukuru sana kwa hili somo, nakuwa namkumbuka sana Dr Slaa katika moja ya maneno aliyoyatamka hotel ya serena. Alisema "Watanzania tuache ushabiki, tuishi maisha halisi". Ulichokiandika mkuu wapo watu watakubeza na kukutukana kwa namna nyingi, ila ifikie mahala tuishi kiuwajibikaji ili tuipate haki yetu. Mihemko ya itikadi za kidini au kisiasa zisitupelekee kuacha kuheshimu mamlaka zinazoendesha nchi.
 
Upuuzi mtupu, kwanini makonda aliamrisha waandishi wa habari wote waporwe zana zao? Si angechukua ya star tv pekee? Kwa akili yako hata mkishinda hiyo kesi ndio kubenea ataporwa ubunge?

Hizo ni mbinu za wahuni na vibaka.Angalieni iko shku atajipaka kinyesi mwili mzima kukwepa soo.
 
Simpendi Makonda lakini ulichoandika ni very right
Kubenea naona bado sana kisiasa..ana mihemko na kutaka
kuonekana yupo serious kuliko hali halisi..

Makonda hafai lakini sheria zinamlinda

Word...hata kama mtu hatumpendi haina maana penye haki tujifanye vipofu. Kubenea kakosea sana kutoheshimu mamlaka. Kuna haja ya UKAWA kuwapatia semina wabunge wao or otherwise wabunge wao watadhalilisha umoja huo muhimu. Kwa maana Watanzania wenye akili tupo na uwa hatuendeshwi na hisia bali logic. Na hili sakata...Kubenea kakosea sana.
 
Tuna mihimili mikuu mitatu kiuongozi kwa mujibu wa Katiba ya JMT. Utawala, Mahakama na Bunge.

Muh. Rais ndiye kiongozi mkuu wa utawala. Vilevile ndiye msimamizi mkuu wa mahakama na bunge. Jaji mkuu na Spika wako chini yake. Kimkoa na kiwilaya, Rais anawakilishwa na Wakuu wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya.

Wakuu Wa wilaya, wakuu Wa mikoa hata ulaya na marekani wapo. Japo majina (title) yanatofautiana, lkn majukumu yao ni kumuwakilisha rais. wabunge kote duniani siyo viongozi Wa kiutendaji (executive).

Nchi zote zina executive, judiciary na legislature. Katika kila nchi executive (Rais na wasaidizi wake) ndiyo watekelezaji Wa sheria kiuongozi. Marekani magavana (tuwaite wakuu Wa mikoa na wilaya) wana nguvu sana kiutendaji.

Licha ya Kubenea kuwa mbunge alipaswa kumheshimu Mkuu Wa wilaya Bila kubishana nae hadharani au kumtukana. Alimuita mhuni na kibaka hadharani.

Makonda ili kuhifadhi ushahidi, aliamua kuteka video camera ya star TV ili ushahidi Wa matusi aliotukanwa usifutwe.

Jiweke katika nafasi ya Makonda. Rais Wa wilaya kutukanwa hadharani. Ikumbukwe kuwa Makonda alikua ameahidi kumpeleka waziri kiwandani Leo.

Kiprotokali baada ya Makonda kuongea na wafanyakazi, Kubenea hakua na haki ya kutaka kuongea baada ya DC. DC aliogopa kuwa maneno ya Kubenea yanaweza chafua hali ya hewa ambayo ilikua imetulia.

Makonda kwa nafasi yake ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika wilaya anayoiongoza. Pangetokea vifo pale kiwandani angelaumiwa Mkuu Wa wilaya. Kubenea anapaswa kulijua hili.

Tabia ya kijeuri ya Kubenea aliionesha siku ya kufungua bunge alipomuomba Kange Lugola kufuta maneno yake. Alitumia lugha ya kibabe sana bila ulazima. Siku hiyo ndiyo nilibaini kuwa Kubenea ana uwezo mdogo wa kujenga hoja. Ni nadra kwake kutumia busara na hekima. Kubenea ajue kuwa kinga anayo bungeni (legislature) siyo uraiani (executive) kwa akina Makonda.

Kubenea alikua na dhamira ya kuwatetea wafanyakazi Wa kiwanda lakini njia aliyoitumia ya jazba na ubabe haikuwa sahihi. Mwl Nyerere aliwahi kuwaambia wanafunzi Wa UDSM walioandamana kuwa "The objectives you have are genuine but the methods you used to achieve your objectives are improper, thus, tarnishing everything".

Tuweke siasa kando. Tuseme ukweli. Katiba ya 1977 ndiyo ituongoze hata kama INA mapungufu. Inawatambua wakuu wa mikoa na wilaya. Wamepewa madaraka kumuweka mtu ndani iwapo hali iliyopo itawalazimu kufanya hivyo. Sheria ni msumeno.

1. Nani alipaswa kumsikiliza nani DC (mtawala wa wananchi) au mbunge (mwakilishi wa wananchi/wanaolalamika)?
2. Tatizo ninaloliona mimi na sehemu moja kutaka kupora madaraka ya sehemu nyingine ili ionekane mwenye sauti ndiye suluhisho la tatizo.
3. Mimi nadhani kulitakiwa DC kuwa pamoja na mbunge katika utatuzi wa mgogoro kwa kumpa nafasi kila interested party katika ule mgogoro na hatimaye kupata suluhisho. Amri pekee huwa hazina suluhisho katika migogoro na kama ingekuwa hivyo huko Morogoro wasingefikia uhasama wa kiasi hicho cha kupigana, kuuana na kuua mifugo.
4. True peace comes after negotiations and not orders/directives.
 
HIVI NI MAKOND HUYUHUYU MFUNGA VIATU VYA RIZ1...na akampiga mzee WARIOBA au kuna mwingine?
 
TULIO ITWA MALOFA NA WAPUMBAV NASI TUMPELEKE NANI kwa COURT
 
At The Same Day Makonda Anamzuia Kubenea Kuongea, Mkuu Wa Wilaya Mvomero Akampa Mbunge Nafas Ya Kuzungumza Na Wananchi.
 
Makonda alikamata camera za waandishi ili kutunza ushahidi au kuppteza ushahidi?
 
Si mmeshapeleka kesi mahakamani, mbona mnajitetea sana mitandaoni?
 
"Bondia,Mtovu wa nidhamu..." labda yangemfaa zaidi lakini hayo mengine yamezidi,acha ashitaki tu.
 
U.S.A hata ulaya au Asia cheo cha mkuu wa mkoa hakipo hata South Africa hakuna cheo cha mkuu wa mkoa hivi vyeo kwa mfano bora wa Uongozi havitumiki ni kama vimepitwa na wakati

dogo acha kukariri, unajua kuwa mkuu wa kikosi, mkuu wa chuo, afisaelimu, hao ni mameneja kwa jina lingine? ulitaka waitwe wakuu wa wilaya na mikoa ndo ujue kama wapo, kazi ipo.
 
Back
Top Bottom