mwongozo junior
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 180
- 65
Tuna mihimili mikuu mitatu kiuongozi kwa mujibu wa Katiba ya JMT. Utawala, Mahakama na Bunge.
Muh. Rais ndiye kiongozi mkuu wa utawala. Vilevile ndiye msimamizi mkuu wa mahakama na bunge. Jaji mkuu na Spika wako chini yake. Kimkoa na kiwilaya, Rais anawakilishwa na Wakuu wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya.
Wakuu Wa wilaya, wakuu Wa mikoa hata ulaya na marekani wapo. Japo majina (title) yanatofautiana, lkn majukumu yao ni kumuwakilisha rais. wabunge kote duniani siyo viongozi Wa kiutendaji (executive).
Nchi zote zina executive, judiciary na legislature. Katika kila nchi executive (Rais na wasaidizi wake) ndiyo watekelezaji Wa sheria kiuongozi. Marekani magavana (tuwaite wakuu Wa mikoa na wilaya) wana nguvu sana kiutendaji.
Licha ya Kubenea kuwa mbunge alipaswa kumheshimu Mkuu Wa wilaya Bila kubishana nae hadharani au kumtukana. Alimuita mhuni na kibaka hadharani.
Makonda ili kuhifadhi ushahidi, aliamua kuteka video camera ya star TV ili ushahidi Wa matusi aliotukanwa usifutwe.
Jiweke katika nafasi ya Makonda. Rais Wa wilaya kutukanwa hadharani. Ikumbukwe kuwa Makonda alikua ameahidi kumpeleka waziri kiwandani Leo.
Kiprotokali baada ya Makonda kuongea na wafanyakazi, Kubenea hakua na haki ya kutaka kuongea baada ya DC. DC aliogopa kuwa maneno ya Kubenea yanaweza chafua hali ya hewa ambayo ilikua imetulia.
Makonda kwa nafasi yake ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika wilaya anayoiongoza. Pangetokea vifo pale kiwandani angelaumiwa Mkuu Wa wilaya. Kubenea anapaswa kulijua hili.
Tabia ya kijeuri ya Kubenea aliionesha siku ya kufungua bunge alipomuomba Kange Lugola kufuta maneno yake. Alitumia lugha ya kibabe sana bila ulazima. Siku hiyo ndiyo nilibaini kuwa Kubenea ana uwezo mdogo wa kujenga hoja. Ni nadra kwake kutumia busara na hekima. Kubenea ajue kuwa kinga anayo bungeni (legislature) siyo uraiani (executive) kwa akina Makonda.
Kubenea alikua na dhamira ya kuwatetea wafanyakazi Wa kiwanda lakini njia aliyoitumia ya jazba na ubabe haikuwa sahihi. Mwl Nyerere aliwahi kuwaambia wanafunzi Wa UDSM walioandamana kuwa "The objectives you have are genuine but the methods you used to achieve your objectives are improper, thus, tarnishing everything".
Tuweke siasa kando. Tuseme ukweli. Katiba ya 1977 ndiyo ituongoze hata kama INA mapungufu. Inawatambua wakuu wa mikoa na wilaya. Wamepewa madaraka kumuweka mtu ndani iwapo hali iliyopo itawalazimu kufanya hivyo. Sheria ni msumeno.