Daraja linaloelea la Tsh. Milioni 158 lazinduliwa Mbulu

Daraja linaloelea la Tsh. Milioni 158 lazinduliwa Mbulu

Ubaya Ubwela

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2024
Posts
2,711
Reaction score
6,474
Wananchi wa vijiji vya Tsawa na Tipri kata ya Gehandu wilaya ya Mbulu mkoani Manyara wamefurahishwa na kukamilika kwa daraja lililojengwa na kwamba baada ya kuteseka kwa miaka mingi na kusababisha kuwa na changamoto ya kukosa kivuko na kusimamisha kuendelea na shughuli za kiuchumi nyakati za mvua.

Daraja hilo ambalo limegharimu Milioni 158 na lenye uwezo wa kubeba Tani 2.4 na linatarajiwa kudumu kwa miaka 70 limezinduliwa na mkimbiza Mwenge kitaifa Ali Ussi Leo Julai 16, ambapo daraja hilo linatajwa litasaidia wanafunzi wa maeneo hayo kupita kwenda shuleni nyakati zote pamoja na wagonjwa kufikishwa kwenye huduma za Afya kwa wakati.
20250716_172356.jpg
 
Wananchi walichohitaji ni daraja. Hiyo kwamba imetumia Mil 158 PCCB na CAG wahangaike nayo. Mwenye mradi kama ni TARURA au TANROAD wathibitishe uhalali wa hicho kiasi maana Hela zilizotumia ni Kodi za Watanznaia wote bila kujali anaisi Mbulu au Mtwara. Hata Mimi ninayeishi Dodoma Kodi ninayolipa ndo imeenda hapo
 
Materials cost 50 million
Upembuzi yakinifu 10 million
Posho za engineers na technician tufanye 20 million
Zinazobaki usiulize tumezinywa ulitaka hela ya kunywa tuitolee wapi
 
Back
Top Bottom