Adha ya foleni inayosababishwa na mizani mpya ya kupimia magari ya mizigo iliyopo eneo la malawi cargo kuelekea daraja la nyerere Kigamboni

Dreamlinerz

Member
Jun 17, 2019
62
77
Kwa muda mrefu barabara ya mandela/shimo la udongo yani kuanzia mzunguko wa magari eneo la mzunguko(round about)ya bandari mpaka mataa ya UHASIBU kulikuwa na foleni kubwa sana kwasababu ya maroli ya makontena,mafuta na mizigo mbalimbali kuegeshwa kiholela katikati ya barabara au maeneo ya watembea kwa miguu(service road)
Hali ilikuwa mbaya sana kwasababu hawa madereva wa maroli ni walikuwa ni watata sana,Hali ilienda hivyo mpaka daraja la kigamboni(Nyerere Bridge)lilivyofunguliwa ndio TRAFIKI wakawa wakali sana wakashughulika na maroli hadi hali ikawa sawa,kwasababu foleni ilikuwa inasababisha ADHA kubwa kwa watumiaji wa njia hiyo kwenda kigamboni.

Sasa tatizo limerudi tena UPYAAA baada ya mizani ya kupimia magari ya mizigo kuanzishwa eneo la MALAWI CARGO,kwa wanaoitumia barabara hii na wanaoenda kigamboni kupitia daraja la Nyerere watakuwa wanaelewa,hali ni mbaya mnoo.

kwa jinsi nilivyoliangalia tatizo hili la foleni hiyo inayosababishwa na maroli yanayokwenda mizani hiyo nimeona pia inaathiri utendaji kazi wa BANDARI yetu kwasababu kunapokuwa na foleni uingiaji na utokaji wa magari ya mizigo bandarini pia unaathirika hivyo kusababisha DELAYS kwa wateja.kwa mfano AZAM anatoa mzigo wa ngano moja kwa moja kutoka melini magari yake inabidi yapange foleni kuelekea kwenye mizani na foleni inapokuwa kali sana inaweza kuchukua hadi dakika 45 mpaka gari lifikie mizani,gari hilo likitoka hapo likapambane na foleni nyingine hadi lifike TAZARA au VINGUNGUTI lifike lishushe mzigo lirudi lipambane na foleni mpaka lifike bandarini tena lipakiliwe mzigo lipate vibali litoke lipange tena foleni ya mizani,na hii ni kwa magari ya mizigo mingine pia kama yanayobeba NONDO,COIL,MBOLEA,CLINKER(material ya kutengenezea CEMENT).

Mamlaka zinazohusika zinabidi ziangalie hii changamoto maana sasa imeleta athari sio tu kwa watumiaji wa hiyo barabara maana unakuta mtu unanasa kwenye foleni kwa zaidi ya saa nzima,sasa inaenda kuathiri hata hata ufanyaji kazi wa bandari.
 
Back
Top Bottom