FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,066
- 40,725
Tofauti ya ferry na darajan ni kwamba darajan abiria wa kwenye gari hawalipi ila ferry gari na abiria wote wanalipa..
Mfano kama una saloon car umepakia abiri wawili, means utalipia gari 1500 na abiria watalipa 200 kila mmoja kama uta opt kupitia ferry. Ila ukipita darajan utalipa 1500 tu kwa saloon car bila kujari umepakia abiria wangapi.. Sasa swali why watu wana opt kupita ferry wakat kuna daraja??
Darajan kwasasa hakufai labda mvua zikwishe.. Kuna mahandaki ya hatari.. Na pia barabara inatope la kuteleza so usipokua vizuri na kua na tairi kipara unaweza kwama au ukapata ajari kwa gari kuteleza.
Kwenye panton changamoto ni kwamba kuna vivuko vitatu (mv magogoni, kigambon, na kazi) wakati zinafanya kazi zote folen huwa hakuna, ila kwasasa kuna changamoto ya panton moja kua bovu (mv kigamboni) hvo kutokana na kuongezeka kwa volume ya magari ambayo yanakwepa kupita darajani kutokana na ubov wa barabara, panton 2 zilizopo zina shindwa handle supply ya magari...
Mimi natumia daraja asubuhi kati ya saa mbili na saa mbili na nusu na huwa natumia muda wa dakika zisizozidi 20 nakuwa nishafika Posta. Jioni natumia njia hio hio kati ya saa kumi na mbili na nusu na saa moja jioni natumia dakika zisizozidi 20 kuvuka darajani.
Ni kweli ile njia baada ya daraja ukitokea mjini au kabla ya daraja ukienda mjini ni mbaya na changamoto lakini huwezi kulinganisha na kero ya kusubiri pantoni. Nikisema nitumie pantoni nafika Kivukoni saa mbili kamili inachukua zaidi ya nusu saa hadi kuingia kwenye pantoni. Baada ya kuingia kuvuka ni kama dakika 5-10 baada ya hapo unatumia tena dakika kama 20 hivi kushuka kwenye pantoni na kuanza kuhangaika na kichochoro cha kutoka Kivukoni hadi uifikie Sokoine Drive.
Ukiamua kutumia daraja ndani ya nusu saa uko Posta ila ukitumia Pantoni ni saa nzima. Kwa Pantoni umbali ninaotumia hadi kufika mjini ni km 10, nikitumia Daraja umbali unakuwa km 14. Kumbuka wakati unahangaika nusu saa nzima kuingina kwenye pantoni gari inakuwa inaunguruma unakula AC kwahio unaweza kuona umbali ni mfupi ila unatumia mafuta mengi kuliko anaezunguka darajani.
Ukitaka kutumia pantoni kwa raha ukiwa unatoka mjini vuka na pantoni kabla ya saa kumi jioni ila ikivuka saa kumi utakaa si chini ya saa nzima hadi kuvuka. Muda mwingi unapotea kwenye kupanda na kushuka, kuvuka majini ni chini ya dakika kumi.