Daraja la Makofia pale mto Ruvu lina matatizo

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,196
13,837
Daraja la Makofia pale mto Ruvu lina matatizo.
Mvua za majuzi zimedhihirisha wasi wasi wangu juu ya usanifu wa daraja hili.

Lakini lazima niweke wazi, sitoi maoni kwa kulaumu , bali kwa nia ya kuweka tahadhari ili hatua zichukuliwe kuokoa hasara dhahiri inayoweza kutokea.

Kwa karibu miaka mitatu au minne mfululizo barabara ya Msata~Bagamoyo imebidi kufungwa kupisha mafuriko ya mto Ruvu.
Mafuriko hayo huwa ni makubwa, kiasi kina kinaongezeka kwa kiasi cha mita tatu hadi tano juu ya wastani uliozoeleka.

Na kama mafuriko yatakuwa wakati wa bamvua, yaani bahari kujaa, halinyaweza kuwa mbaya zaidi.
Nimeshuhudia na si mara moja bahari ikigeuza mkondo wa maji pale daraja la chuma linalokatiza mto Ruvu!

Na hapo ndo wasi wasi wangu.

Najiuliza je, usanifu wa barabara umetilia maanani haya yote?
Barabara inayopita bonde hili la Ruvu inaweza kuwa kama kizuio kikubwa cha mto hivyo kutengeneza bwawa, na bwawa hili likijaa na maji.kupita juu ya barabara, huo unakuwa mwisho wa barabara mpya ya Msata~Bagamoyo.

Pengine ni wasi wasi wangu tu, wataalam wa ujenzi TANROADS hebu tondoleeni huu wasi wasi.
 
Maoni mjarabu haya.
Wwasiporekebisha tuta na daraja kwa kuliinua, litakuwa linafungwa kila masika ijapo!
 
Hawa makandaras hawaoni aibu yani hadi kwao mkuu wa kaya aliyewapa tender bado wanajenga chini ya kiwango....
 
Hawa makandaras hawaoni aibu yani hadi kwao mkuu wa kaya aliyewapa tender bado wanajenga chini ya kiwango....
Tatizo si la mkandarasi, ni la yule aliyebuni mradi.
Ndio maana ujumbe huu unawahusu sana TANROADS.
Ni muhimu sana ubunifu wa kihandisi ukarejewa hasa kipande cha pale Makofia hadi kuvuka daraja lenyewe juu ya mto Ruvu.
 
Back
Top Bottom