Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,608
- 4,266
Hilo swali kamuulize fisadi Lowasa na Genge lake!
Huyo Lowassa mnamwota usiku? Hilo daraja na wizi ulioambatana na ujenzi wake (kama ulikuwepo) vinahusiana vipi na Lowassa?
Genge la wezi analo mkulu maana Kila ninapomsikia Mwigulu Nchemba anadai kuwa Magufuli hana marafiki kwa hiyo hataibebesha mzigo serikali na wala baraza lake la mawaziri halitakuwa kuuuubwa kama lililopo sasa. Anadai baraza la sasa hivi ni kubwa sana na gharama kwa serikali kwa sababu rais alitakiwa kulipa fadhila kwa waliomsaidia kuingia madarakani. Sasa ilikuwaje mwaka 2010 wakamrudisha huyo huyo madarakani hata baada ya kuona ni mlipa fadhila? Tatizo chuki yenu dhidi ya Lowassa inawafanya 'mumtukane' Rais wenu bila hata kujitambua. Hata Magufuli mwenyewe huwa 'anamtukana' rais wake aliyemteua kwa kumwita 'lijizi na lifisadi' (lililotufikisha hapa tulipo).
Ila kwa hilo la fadhila namuunga mkono huyo jamaa maana JK anajitahidi kuwa na huruma kwa marafiki zake. Naamini hata atakapokuwa analihutubia taifa siku ya jumamosi tarehe 24/10/2015, siku moja kabla ya uchaguzi kuna watakaoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali...
Mwaka huu kuna mambo!