Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi

Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024
1.jpg


j3.jpg


Kikwete%2BBridge-753512.JPG


3854207679_f0ed0caed0_b.jpg


Ujenzi wa Daraja la Kikwete katika mto Malagarasi mkoani Kigoma umekamilika. Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma aliweza kutembelea eneo hilo na kujionea magari yakiwa yanapita katika daraja hilo.

Daraja.jpg

Sehemu ya barabara pamoja na Daraja la Kikwete kama inavyoonekana hivi sasa baada ya kukamilika kwa ujenzi wake.

Kampuni ya M/S Hanil Engineering and Construction Company Limited kutoka Korea ya Kusini iliingia mkataba na kuanza ujenzi wa daraja hilo mwezi Desemba 2010 na kutakiwa kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Desemba 2013. Mradi huo unajumuisha ujenzi wa madaraja matatu yenye jumla ya urefu wa meta 275 pamoja na barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 48 kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 64 ambazo ni sawa na Shilingi bilioni 90 za Kitanzania zilizotolewa na Benki ya Exim ya Korea ya Kusini kwa asilimia 90 na kiasi kilichobaki kikiwa ni fedha za ndani.

Akitoa maelezo ya mradi huo Mhandisi Yu Sing kutoka kampuni ya Hanil Engineering alimfahamisha Waziri Magufuli kuwa, Mradi huo umegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ambayo ndiyo iliyokamilika ni ujenzi wa madaraja matatu yenye urefu wa meta 25, meta 200 na meta 50 pamoja na kilometa 11 za lami. Sehemu ya pili ni ujenzi wa kilometa 37 za lami ambazo ndizo zinazoendelea kukamilishwa kwa sasa.
WZ_na_RC_Kikwete_Bridge.jpg

Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Msataafu Issa Machibya (kulia) pamoja na Watendaji mbali mbali wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi mkoani Kigoma.

Baada ya kutembelea eneo hilo la mradi, Mheshimiwa Magufuli alielezea kuridhishwa kwake na utendaji wa mkandarasi huyo kutokana na kukamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ya kwanza kwa mujibu wa mkataba na kwa viwango vya hali ya juu. Nimeridhishwa na utendaji wa mkandarasi huyu na hasa kwa jinsi alivyoweza kumaliza sehemu hii ya kwanza kwa muda mzuri na viwango vya hali ya juu alibainisha Mheshimiwa Magufuli.

Kwa muda mrefu usafiri katika eneo hilo ulikuwa ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya mkoa wa Kigoma hasa nyakati za mvua kutokana na kukosekana kwa daraja la uhakika. Kwa hivi sasa kumenza kuonekana ongezeko kubwa la magari kati Manyoni Itingi Tabora hadi Kigoma kupitia katika Daraja hilo la Kikwete hali ambayo awali ililazimu kupitia barabara ya Manyoni Singida - Nzega Kahama Nyakanazi Kibondo Kasulu hadi Kigoma.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya aliyeambatana na Waziri wa Ujenzi katika ziara hiyo, aliishikuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma kwa kutimiza ahadi ambayo imekuwa ikisuburiwa kwa muda mrefu. Kukamilika kwa mradi huu pamoja na mingine mingine ambayo inaendelea kujengwa katika barabara ya Kigoma kuelekea Tabora hadi Manyoni mkoani Singida, ni ufumbuzi mkubwa wa matatizo yaliyokuwa yakikwamisha maendeleo katika ukanda huu wa magharibi, hii ni fursa ya pekee kwa amendeleo ya ukanda huu wa Maharibi alimalizia Mhe. Machibya.
WZ_na_RC_juu_ya_Daraja_Kikwete.jpg

Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Msataafu Issa Machibya (wa pili kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto) wakipita kwa pamoja na Watendaji mbali mbali katika Daraja la Kikwete.
 
Hiviiiiii hilo ni daraja au kidaraja? Hata magari hayawezi kupishana kabisa kwa kuwa ni 2 ways at least 4 ways will be a good plan na ndio maana foleni kila kukicha. That bridge is total the waste of money and time yaani hakuna la kujisifia zaidi ni ----- mtupu... 4 ways will be great and super miji inapanuka kwa haraka na hicho kidaraja kitaua sana tu hapo kuanzia waenda kwa miguu/ pikipiki/ baiskeli na magari aina zoteeee. Kwa kifupi hapo ni 0+ hakuna jipya kabisaaaaa ni kama enzi zileeeee za Mwalimu JK NYERERE
 
Hiviiiiii hilo ni daraja au kidaraja? Hata magari hayawezi kupishana kabisa kwa kuwa ni 2 ways at least 4 ways will be a good plan na ndio maana foleni kila kukicha. That bridge is total the waste of money and time yaani hakuna la kujisifia zaidi ni -- mtupu... 4 ways will be great and super miji inapanuka kwa haraka na hicho kidaraja kitaua sana tu hapo kuanzia waenda kwa miguu/ pikipiki/ baiskeli na magari aina zoteeee. Kwa kifupi hapo ni 0+ hakuna jipya kabisaaaaa ni kama enzi zileeeee za Mwalimu JK NYERERE
Ujuaji mwingine unaoneka hamnazo! Sasa huko porini waweke 4lanes ili iweje? Foleni...seriously!
 
Ni kodi zetu, fananisha na kiasi mlichoiba je tungepata madaraja mangapi
 
Kulikuwa haina maana kuliita kikwete bridge badala ya jina lake la asili MALAGARASI BRIDGE
 
Yaani kidaraja cha mita 200 tu kelele nyiiingi, nilidhani ni km 2!
 
Mwanangu hata kama uko ukawa, sasa naona umepitiliza, dahh, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Hata hii nayo ni hatua, acha kuponda swala la kujiuliza ni hatua ya namna gani, maana hata kinyonga naye ana mwendo..
hii ni hatua, tena ya kujivunia.

Ila Taifa lina changamoto nyingi, na kubwa sana kulinganisha na mafanikio tunayoonyeshwa sasa hivi.

Zipo changamoto ambazo zitahitaji zaidi ya miaka 20 kuzitatua na zinahitaji viongozi wenye uelewa mpana na uzalendo wa juu, infact tunahitaji watu wenye maono na mtazamo mwingine tofauti na hawa tuliowazoea.

Hiviiiiii hilo ni daraja au kidaraja? Hata magari hayawezi kupishana kabisa kwa kuwa ni 2 ways at least 4 ways will be a good plan na ndio maana foleni kila kukicha. That bridge is total the waste of money and time yaani hakuna la kujisifia zaidi ni ----- mtupu... 4 ways will be great and super miji inapanuka kwa haraka na hicho kidaraja kitaua sana tu hapo kuanzia waenda kwa miguu/ pikipiki/ baiskeli na magari aina zoteeee. Kwa kifupi hapo ni 0+ hakuna jipya kabisaaaaa ni kama enzi zileeeee za Mwalimu JK NYERERE
 
Mr Chin waonesha daraja, wakati watoto wanazaliwa na kukua bila kulifahamu bomba la maji safi na salama?
 
Last edited by a moderator:
Nyie wote kumbe hamjui deal zinavyochezwa ee? Sasa ngoja niwaambie kitu. Katika mali nyingi zinazovunwa na wageni nyie mnaambulia barabara alafu mnaanza kulia lia. Sehemu yoyote ukiona inajengwa barabara ndefu ujue uko inapoelekea kuna deal kubwa kama si madini basi gas au mafuta hivyo wawekezaji wanajijengea wenyewe barabara mfano Dar to Mwanza(ukanda wa madini), dar to mtwara(gas) sasa hii ya kigoma subirieni mtakuja sikia ya lake tanganyika siku si nyingi na uko ziwa tanganyika wamejaa watafiti wa kigeni kila kukicha wanajifanya wazamiaji
 
Sasa daraja la mita 200 ndio linazinduliwa na presidential convoy? Mbona mkuu wa wilaya alitosha kabisa!

Kwahio daraja la ukubwa gani linastahili kufunguliwa na President na convoy yake?
 
Back
Top Bottom