Daraja la Kigamboni limefikia wapi?

samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,594
4,798
Natumaini mnaendelea na weekend yenu kwa utulivu huku tukidigest majipu yaliyotumbuliwa week nzima.

Nataka tu kujua maendeleo ya lile daraja la kigamboni, limefikia wapi? Nakumbuka Mh Rais wakati huo akiwa waziri wa ujenzi aliagiza kandarasi ahakikishe linaanza kupitika september 2015 ila mpaka leo naona kimya.. Kunani kinaendelea? Ujenzi umekwama? Na kama haujakwama nini basi kinasubiriwa ili daraja liweze kuanza kutumika?

Binafsi ni mdau huko kigamboni na nina kiplot changu mitaa ya kibada nilianza msingi ila shuruba za pale feri kuvuka na gari zilinishinda nikaamua nisubiri kwanza daraja lifungiliwe ili niweze kumalizia kibanda changu na kuachana na maisha ya kupanga.

Basi si vibaya kama kuna mtu ana updates akaniwekea hapa kwani ni siku mingi kidogo na hatujui nini kinaendelea, ukipata kapicha ukatupia sio mbaya pia..

Wenu mdau.. Kigamboni resident to be.
 
Daraja liko hatua nzuri na mwisho mwisho na kuna barabara ya lami kutokea Kurasini via darajani mpaka kilometa moja kuingia vijibweni na sasa wanaendelea ujenzi wa barabara kuunganisha na ya kisiwani, in Short Kuna PROGRESS YA MAANA SANA

Picha siku ingine
 
Bora uhamie Kibada nije kukutembelea nile maembe..........
Subiri majirani watatuhabarisha kama daraja lipo au lah........

Umeona eeeh? Wacha nisubiri updates, Magufuli kawatisha mabosi wanagoma kusaini likizo aisee.. Xmass mwaka huu tunailia huku huku porini:(
 
Daraja liko hatua nzuri na mwisho mwisho na kuna barabara ya lami kutokea Kurasini via darajani mpaka kilometa moja kuingia vijibweni na sasa wanaendelea ujenzi wa barabara kuunganisha na ya kisiwani, in Short Kuna PROGRESS YA MAANA SANA

Picha siku ingine

Asante mkuu.. Kwa hiyo barabara za kuunganisha kwa upande wa kule kigamboni zishaanza kujengwa? Shida ingine itakua pale kurasini manake yale malori yanayotoka bandarini sijui itakuwaje.. Ila naskia kuna mpango wa kuweka ka fly over pale
 
Enzi za kucheka cheka zimekwisha, kwa mzinza ni kazi tu hilo daraja litakwisha mwaka huu jiandae kwenda kumalizia kichuguu chako.
 
Asante mkuu.. Kwa hiyo barabara za kuunganisha kwa upande wa kule kigamboni zishaanza kujengwa? Shida ingine itakua pale kurasini manake yale malori yanayotoka bandarini sijui itakuwaje.. Ila naskia kuna mpango wa kuweka ka fly over pale

Kweli kabisa. Lazima waondoe mwingiliano na malori ya bandarini
 
Back
Top Bottom