Daraja jipya la Nyerere lipewe ulinzi wa kutosha

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,988
1,209
Habari wana jamvi.
Nimelazimika kuandika uzi huu baada ya kuona yanajiri katika daraja letu jipya.

Jana nilienda Kimbiji kuangalia kiwanja sasa tulichelewa sana kurudi mpaka tunafika darajani pale ilikuwa kama saa 1.30 usiku.

Kulikuwa na magari mengi yamepaki nadhani wanachi walikuwa wameenda kutembelea daraja hilo lenye historia katika ukanda huu wa afrika ya mashariki na kati.

Nilipoangalia nikaona kuna askari mmoja wa kampuni za ulinzi na bunduki yake ya rifle.
Na upande wa pili nako pia kuna askari kama huyo kilichonipa mashaka katika ya daraja watu wamepaki magari wamewasha hazadi wameshuka wanapiga picha.

Siyo mbaya sana wananchi wanafurahia daraja lao lakini tunaamini vipi hawa watu akitokea mtu mbaya na kufanya hujuma katika daraja hilo atagundulika kweli.

Hivyo naziomba taasisi zinazohusika ziangalie daraja kama ni nyenzo muhimu ni miundo mbinu ambao umebadilisha kabisa eneo hilo na kulipa thamani.

Naomba kuwasilisha.
 
Hapana ninamaanisha daraja la Julius Kambarage daraja la kigambini
 
Baada ya Muda kigamboni itakufa. Hata La Mkapa walisema hivyohivyo ila La Mkapa lipo hewani hadi leo. Pia vizazi vijavyo, havifahamu issue za Kigamboni wao Nyerere ndio wataikuta.
Ni kazi ngumu sana kubadilisha jina la daraja is kigamboni kuwa la nyerere kama ilivyo viwanja vya sabasaba kuitwa cha Nyerere. Tutaita hivyo kwenye maandishi tu
 
Baada ya Muda kigamboni itakufa. Hata La Mkapa walisema hivyohivyo ila La Mkapa lipo hewani hadi leo. Pia vizazi vijavyo, havifahamu issue za Kigamboni wao Nyerere ndio wataikuta.

Viwanja vya sabasaba hilo jina litakufa lini?
 
Baada ya Muda kigamboni itakufa. Hata La Mkapa walisema hivyohivyo ila La Mkapa lipo hewani hadi leo. Pia vizazi vijavyo, havifahamu issue za Kigamboni wao Nyerere ndio wataikuta.
Kigamboni haiwezi kufa labda kama unamaanisha jina la daraja
 
Jina la daraja mkuu. Vizazi vijavyo havitalikuta daraja likiitwa Kigamboni. Ule mji utadumu, make ndio akina CHENGE wanachukua site huko kwa sasa.
Mkuu ni hatari baada ya miaka miwili huko kutabadilika sana kunajengwa balaa na barabara ipo katika mpango wa kuwekwa rami hadi buyini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom