Dar: Wanafunzi 4 wa Chuo Kikuu cha Kampala kortini kwa kumkashifu Rais Magufuli kupitia WhatsApp

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740
Wanafunzi kortini kwa kumkashifu Rais Magufuli

Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala(KIU) kampasi ya Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shitaka la kusambaza picha za kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Washitakiwa hao ni Amenitha Kongo(19), Maria Tweve (20), Agnes Gabriel(21) na Anne Mwansasu(21), ambapo wamepandishwa mahakamani hapo leo na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kuchapisha picha ambazo zinaonyesha Rais Magufuli akiwa amevaa hijabu kama mwanamke wa Kiislamu na kuzisambaza kwenye mtandao huo wa WhatsApp, huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kitimiza masharti ya dhamana.

Chanzo: Mwananchi
 
Wanafunzi kortini kwa kumkashifu Raisi Magufuli

Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shtaka la kusambaza picha za kumkashifu Rais John Magufuli kupitia Mtandao Wa kijamii wa WhatsApp.[HASHTAG]#Mwananchileo[/HASHTAG]

bora arudie ubunge wake tu awe anamalizana na watu wake wa hukohuko tu
 
Huyu mtukufu raisi asiesemwa wala kukosolewa, pure dictatorship in Tanzania. Kwanza alizima bunge msione wanachoikosoa serikali yake, kagandamiza vyombo vya habari, now he is cracking individuals with different views na upinzani. Aliapa kutokomeza upinzani, kwa mwendo huu come 2020/5 kutakua na chama kimoja ambacho kutoka madarakani hadi tupigane. Maoni tu mjomba nchumali hutaniwi?
 
"Mi nimeelewa sana sasa kwa nini operation UKUTA iliandaliwa. Makamanda waliona mbaali mno toka mwanzo kazi ipo"
 
Huyu mtukufu raisi asiesemwa wala kukosolewa, pure dictatorship in Tanzania. Kwanza alizima bunge msione wanachoikosoa serikali yake, kagandamiza vyombo vya habari, now he is cracking individuals with different views na upinzani. Aliapa kutokomeza upinzani, kwa mwendo huu come 2020/5 kutakua na chama kimoja ambacho kutoka madarakani hadi tupigane. Maoni tu mjomba nchumali hutaniwi?
Mstari wa mwisho .ahahhaaaa
 
Baba mwenye nyumba huwa hakosolewi ila hupewa ushauri tu ..au wewe umewahi kumkosoa baba ako?
Acha kulinganisha baba na urais, ili uwe baba kuna tendo unafanya na mwenzako wa jinsia tofauti na ili uwe rais kuna utaratibu unapitia kwa mujibu wa sheria, kwa hiyo baba na urais ni vitu viwili tofauti havipaswi kulinganishwa. Baba ataheshimiwa kwa mujibu wa mila zetu na desturi na rais ataheshimiwa kwa mujibu wa katiba na sheria zetu.
 
Wanafunzi kortini kwa kumkashifu Rais Magufuli

Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shtaka la kusambaza picha za kumkashifu Rais John Magufuli kupitia Mtandao Wa kijamii wa WhatsApp.
Kazi ipo awamu hii maana Polisi washajua jamaa hakosei na akikosea hatakiwi kukosolewa bali watu wapige vigelegele na vifijo!. Kama Polisi washaamua hivyo basi tutakaoenda jela awamu hii tutakuwa wengi
 
Back
Top Bottom