DAR: Wafanyabiashara watatu wahukumiwa kifungo cha miaka 2 jela kwa hatia ya kusafirisha dhahabu bila kibali

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
DAR: Mahakama ya Kisutu imewahukumu wafanyabiashara watatu kwenda jela miaka 2 au kulipa faini ya Shs. milioni 9 (milioni 3 kila moja) baada ya kuwakuta na hatia ya kusafirisha madini ya dhahabu yenye thamani ya milioni 507 bila kibali.

Mhakama pia imetaifisha madini hayo yenye uzito wa kilo 6.242 kuwa mali ya serikali

Waliohukumiwa ni mfanyabiashara Mashaka Lucas, Japhari Hussein na Akeef Mohamed

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi alisema hukumu hiyo imezingatia watuhumiwa kukiri kosa hilo na kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda kosa hilo,

Chanzo: Millard Ayo
 
sasa dhahabu wanarudisha au wanaenda nayo kama vipi wamuhukumu huyo wa nzanzibar fasta baba mwenyenyumba hizo fedha anaziitaji
 
sahihi mara yao ya kwanza kukamatwa na kushitakiwa!
 
sasa dhahabu wanarudisha au wanaenda nayo kama vipi wamuhukumu huyo wa nzanzibar fasta baba mwenyenyumba hizo fedha anaziitaji
duh, hv we umesoma kweli post kabla ya kuchangia au umekurupuka tu, jaribuni kuficha ujinga wenu kidogo bac dah
 
Kosa la kusafirisha dhahabu ya zaid 500 M kinyume cha Sheria Lina adhabu ndogo kuliko kukojoa eneo lisiloruhusiwa!
 
Someni post jamani, Hakimu kasema amezingati adhabu yake kuwa jamaa wamekiri kosa (hawakusumbua Mahakama) pia ni kosa lao la kwanza.

Jee ukimtia Mimba Mwanafunzi Halafu ukakiri kosa haraka bila ya kusumbua Mahakama Halafu Ikawa kosa lako la kwanza inakuaje hapo?
 
Back
Top Bottom