In 2009, aina za mabasi makubwa za kisasa zenye rangi nyekundu ziliwekwa kwenye mabarabara za jiji ya Nairobi. Kuzitumia, wasafiri wangehitajika hata kutumia kadi, yani badala ya kumpa kondakta pesa, wewe ungeswipe kadi yako tu pale na hivyo kuweza kusafiri. Lakini kuna wadau kwenye sekta ya usafiri ambao walilipinga vikali mfumo huo, wakidai ingewakandamiza kibiashara na vijana wengi wangepoteza ajira.Baadaye, sijui haswa ni njia gani hizo mabasi zilipata kuondolewa, lakini kulikuwa na maelewano ya kwamba kuwe na ratiba za kuondolewa kwa hizi magari madogo za usafiri aina ya nissan vans na kuwa replaced na mabasi makubwa zenye uwezo wa kuwabeba angalau abiria 30 , ili kupunguza msongamano kwenye barabara za miji mikuu za Kenya.