Waandishi wa habari walioshiriki Press Conference ya Lissu na kuandika habari zake wameitwa Polisi kuhojiwa. Taarifa za awali zinaeleza kuwa baadhi yao watashtakiwa kwa kusambaza habari za uchochezi kinyume na Sheria ya huduma za habari kifungu cha 47(1), ambapo wakipatikana na hatia waweza kufungwa miaka mitatu hadi mitano jela, faini ya milioni 20 au vyote kwa pamoja.
[HASHTAG]#Mytake[/HASHTAG]:
Inasikitisha kuona nchi yetu imefika hapa. Waandishi hawapo huru tena. Inabidi waandike yanayofurahishawatawala tu, na kuacha kuandika yanayowakera. Hata kama ni ya kweli lakini yakiwaudhi watawala ni kosa. Naanza kuona habari nyingi za wapinzani zikikosa coverage kwa waandishi kuhofia kushtakiwa. Hii ni dalili mbaya sana katika ukuaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini. Inasikitisha sana.!
Nakubaliana na wewe ni vibaya kuzuwia baadhi ya habari zisisambae vivyo hivyo sikubaliani na uhuni wa waandishi wa habari kuamua habari ya nani waisambaze.Kama ilivyovibaya kutumia mamlaka kuzuwia habari ni ubaya wa kiwango kile kile kutumia kalamu yako kuzuwia habari za wengine.
Kwa kuwa ni vibaya kuandika habari zinazosifu watawala tu kwa nini baadhi yetu wanadhani ni vizuri kuandika habari zinazopinga kila kitu cha watawala na kupendesha habari za wasiokubaliana na watawala?
Unachopanda ndicho unachovuna.