DAR: Tundu Lissu aendelea kushikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana. Waandishi watishwa!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Wakuu,

Nipo hapa Central na hali inaanza kuwa mbaya.

Polisi wametanda na wametangaza rasmi vita na waandishi wa habari ambao wamejaa tele eneo hili kujua kinachotokea.

Maafisa wa Polisi wamekutana na waandishi na kuwapa onyo la mwisho na kuwambia wasiwalaumu kwa kitakachowakuta.

Wamesema wao kama Polisi hawataki ushirikiano na Media katika hili na hata waandishi walipolalamika juu ya utaratibu wametishiwa kuondolewa kwa nguvu.

Lissu alikamatwa Uwanja wa Ndege akiwa anaelekea Kigali, habari zaidi soma =>Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akamatwa akiwa uwanja wa ndege wa Dar akielekea Kigali

10482113e75c9331eeb92ad963d42e71.jpg

Nipo hapa, nitawapa updates zaidi

=====

UPDATE:

Hatimaye waandishi wameweza kusogelea kituo.

Wanasheria wanajipanga kwenda Mahakama Kuu kutaka Lissu afikishwe mahakamani. Wanaongozwa na Wakili Msomi, Fatma Karume. Lissu kakataliwa dhamana!

Lissu anadaiwa kufanya uchochezi ila haijaelezwa ni uchochezi gani.

Wanasheria wanataka afikishwe mahakamani ili ielezwe ni uchochezi gani kafanya.

7b158a5be7373396722cc3b6b9d20b2e.jpg

Dar es Salaam. Wakili wa Mbunge wa Singida Mashariki, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha CHADEMA Mheshimiwa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema polisi walikataa kumpa dhamana mteja wake jana jioni mara baada ya kukamatwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na Mwananchi, Karume alisema baada ya kufikishwa polisi, Lissu alitakiwa kuandika maelezo na kupewa onyo kwa kosa la uchochezi.

“Lakini cha ajabu mpaka sasa hivi hatujaambiwa Lissu kamchochea nani, kosa la uchochezi lazima lilete madhara au uhalifu kwa wengine na ni lazima liwe la uhalifu.” Amesema

Amesema hata walipouliza nani anayeweza kuruhusu mteja wake apate dhamana hiyo waliambiwa imezuiwa kwa amri kutoka juu.

Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) alikuwa akielekea Kigali, Rwanda, katika mkutano wa wanasheria wa Afrika.

Karume amesema uchochezi lazima liwe ni jambo la uhalifu na mpaka sasa polisi hawajamwambia Lissu aina hiyo ya uchochezi.

“Hili ni jambo la kisiasa, Lissu amezuiwa kwenda kwenye mkutano wa wanasheria wa Afrika, jambo hilo linawafanya hata wanasheria wote wa Afrika kujua mwenzao kakamatwa na Serikali,” amesema.

Kwa mujibu wa Karume, Lissu amewapa ujumbe Watanzania akisema Aluta Continua, na kuwa yupo sawa

Chanzo: Mwananchi

Yahusu Antipas Tundu Lissu Mughwai;

Kwanza kabisa shukrani za pekee sana ziende kwa Wakili Fatma Karume wa IMMA Advocates ambaye tangu jana alipofikishwa Tundu Lissu Central Police Station amekuwepo, na leo tumekuwa naye tukijaribu kupigania haki za Tundu Lissu kwa pamoja.

Huyu ni Binti wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume; na ni mtu mwenye msimamo thabiti usioyumba kwa lile analoliamini na pamoja na kwamba siku zote amekuwa mstari wa mbele kupigania Utawala wa Sheria na Demokrasia, na katika hili la Tundu Lissu ameamua kwamba hatapumzika mpaka pale kila iliyo haki ya Tundu Lissu kisheria, inapatikana.

Ameguswa MNO baada ya kuona Rais wa Chama Chake, TLS, amekamatwa na hajafikishwa Mahakamani kwa haraka.

Wakati naandika taarifa hii, Wakili Fatma Karume anapigana ili maombi ya Harbeas Corpus aliyoyaandaa yeye mwenyewe ili kuiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam iliamuru Jeshi La Polisi Tanzania aidha kumfikisha Mahakamani au kumuachia Tundu Lissu, yasikilizwe kwa haraka.

Leo hii tulifika Central Police Station na Wakili Karume, na baada ya kuona hakuna dalili za Jeshi hilo kumpatia dhamana wala kumfikisha Mahakamani kwa muda ule; haraka ikaandalia hati ya maombi niliyoyataja hapo juu. Tunakusudia kuwa-serve nakala Jeshi la Polisi Makao Makuu leo hii.

Tunashukuru Chama cha Mawakili Afrika Mashariki kwa kushirikiana nasi na tunategemea watatoa tamko stahili kuhusiana na kukamatwa na kuendelea kushikiliwa rasi wa TLS, Tundu Lissu.

Tunashukuru pia Chama Chetu cha Mawakili Tanganyika, TLS, kwa kutoa tamko lisilomung'unya maneno kuhusu kukamatwa na kuendelea kushikiliwa Rais Tundu Lissu.

Tunaamini tutaendelea kupata support kutika pande zote ili hatimaye Tundu Lissu aidha afikishwe Mahakamani kwa haraka ama apatiwe dhamana kwa mujibu wa sheria; iwapo Jeshi la Polisi bado halijakamilisha taratibu za Upelelezi (wa Kosa/Makosa yoyote yale wanayomtuhumu nayo Tundu Lissu). Tunataraji kwamba kwa kukamatwa kwake Uwanja wa Ndege; hiyo inamaanisha Jeshi la Polisi limekamilisha taratibu zote za kipelelezi na kujiridhisha kwamba kuna Makosa ya Jinai ili kuonesha kwamba "they investigated first, and arrested later" na si vinginevyo. Iwe iwavyo, tutaendeleza juhudi za kisheria kuhakikisha Tundu Lissu anapatiwa dhamana au anafikishwa mahakamani mapema iwezekanavyo; kwa kuwa huyu si tu ni raia mwenye haki zote za Kikatiba, bali ni RAIS WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA.

Tutawapa taarifa zaidi.
VIDEO: Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani
 
KARUME.jpg

Dar es Salaam. Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema polisi walikataa kumpa dhamana mteja wake jana jioni mara baada ya kukamatwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na Mwananchi, Karume alisema baada ya kufikishwa polisi, Lissu alitakiwa kuandika maelezo na kupewa onyo kwa kosa la uchochezi.

“Lakini cha ajabu mpaka sasa hivi hatujaambiwa Lissu kamchochea nani, kosa la uchochezi lazima lilete madhara au uhalifu kwa wengine na ni lazima liwe la uhalifu.” Amesema

Amesema hata walipouliza nani anayeweza kuruhusu mteja wake apate dhamana hiyo waliambiwa imezuiwa kwa amri kutoka juu.

Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) alikuwa akielekea Kigali, Rwanda, katika mkutano wa wanasheria wa Afrika.

Karume amesema uchochezi lazima liwe ni jambo la uhalifu na mpaka sasa polisi hawajamwambia Lissu aina hiyo ya uchochezi.

“Hili ni jambo la kisiasa, Lissu amezuiwa kwenda kwenye mkutano wa wanasheria wa Afrika, jambo hilo linawafanya hata wanasheria wote wa Afrika kujua mwenzao kakamatwa na Serikali,” amesema.

Kwa mujibu wa Karume, Lissu amewapa ujumbe Watanzania akisema Aluta Continua, na kuwa yupo sawa

Chanzo: Mwananchi

My Take
Akikamatwa na Kuachiwa

Bavicha: Jamaa Jembe hamuwezi wanacheza Ngoma yake

Akibanwa na Kukosa Dhamana

BAVICHA: Maamuzi yametoka juu ifike kipindi tuheshimu Mahakama hazitakua upande wenu kila siku Sheria ni Msumeno.
 
View attachment 547248 Dar es Salaam. Wakili wa Tundu Lissu,
Fatma Karume amesema polisi walikataa kumpa dhamana mteja wake jana jioni mara baada ya kukamatwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na Mwananchi, Karume
alisema baada ya kufikishwa polisi, Lissu alitakiwa kuandika maelezo na kupewa onyo kwa kosa la uchochezi.

“Lakini cha ajabu mpaka sasa hivi
hatujaambiwa Lissu kamchochea nani,
kosa la uchochezi lazima lilete madhara au uhalifu kwa wengine na ni lazima liwe la uhalifu.” Amesema

Amesema hata walipouliza nani
anayeweza kuruhusu mteja wake apate dhamana hiyo waliambiwa imezuiwa kwa amri kutoka juu

Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha
Wanasheria wa Tanganyika, (TLS)
alikuwa akielekea Kigali, Rwanda, katika mkutano wa wanasheria wa Afrika.

Karume amesema uchochezi lazima liwe ni jambo la uhalifu na mpaka sasa polisi hawajamwambia Lissu aina hiyo ya uchochezi.

“Hili ni jambo la kisiasa, Lissu amezuiwa kwenda kwenye mkutano wa wanasheria wa Afrika, jambo hilo linawafanya hata wanasheria wote wa Afrika kujua mwenzao kakamatwa na Serikali,” amesema.

Kwa mujibu wa Karume, Lissu amewapa ujumbe Watanzania akisema Aluta Continua, na kuwa yupo sawa.

My Take
Akikamatwa na Kuachiwa

Bavicha: Jamaa Jembe hamuwezi wanacheza Ngoma yake

Akibanwa na Kukosa Dhamana
BAVICHA: maamuzi yametoka juu ifike kipindi tuheshimu Mahakama hazitakua upande wenu kila siku Sheria ni Msumeno.
Kwani waliomnyima dhamana ni mahakama?Unamkamataje mtu wakati hata upelelezi hujaanza???
 
Acha upuzi ww hujuu sheria kaa kimya nani kasema mahakama huwa inakua upande wa Lissu ndio hushinda kesi, ushawai ona wapi hiyo na swala la mtubkupewa dhaman ni haki yake ya msingi kwani hilo kosa lina dhamana.

Sio umnyime mtu dhamana kwa kusema maagizo kutoka juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waandishi wa habari walioshiriki Press Conference ya Lissu na kuandika habari zake wameitwa Polisi kuhojiwa. Taarifa za awali zinaeleza kuwa baadhi yao watashtakiwa kwa kusambaza habari za uchochezi kinyume na Sheria ya huduma za habari kifungu cha 47(1), ambapo wakipatikana na hatia waweza kufungwa miaka mitatu hadi mitano jela, faini ya milioni 20 au vyote kwa pamoja.

[HASHTAG]#Mytake[/HASHTAG]:
Inasikitisha kuona nchi yetu imefika hapa. Waandishi hawapo huru tena. Inabidi waandike yanayofurahishawatawala tu, na kuacha kuandika yanayowakera. Hata kama ni ya kweli lakini yakiwaudhi watawala ni kosa. Naanza kuona habari nyingi za wapinzani zikikosa coverage kwa waandishi kuhofia kushtakiwa. Hii ni dalili mbaya sana katika ukuaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini. Inasikitisha sana.!
 
Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, wamewafukuza waandishi wa habari waliokuwa wakisubiri taarifa ya kukamatwa kwa Rais wa TLS, Tundu Lissu.
 
Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, wamewafukuza waandishi wa habari waliokuwa wakisubiri taarifa ya kukamatwa kwa Rais wa TLS, Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom