Dar Traffic update - Feb 17, 2014: Kuna Foleni kubwa Morogoro road

benbry

Senior Member
Apr 3, 2012
183
54
Hivi serikali haioni ni kwa kiasi gani inapoteza kwa sababu ya foleni ktk hii barabara? tunajua inatengenezwa fine, ila watengenezaji kwa nini wanaitengeneza kibabe hivyo? nani anaijua foleni ya kwenda mjini hasa maeneo ya kuivuka kimara? kwa nini pale kimara wasipanue kile kipande haraka ili magari yapite kwa urahisi? Nina hasira kupitiliza.
 
Nilikuwa naishi Mbezi lakini kwa sababu ya foleni nimechukua vichumba viwili kwenye ka guest fulani hapa Sinza. Nilikuwa nimechoka kuondoka nyumbani saa kumi asubuhi na kurudi saa sita usiku!

Nasubiri wamalize ndio nirudi Mbezi Makondeko.
 
Miji ya Tanzania ni ya ajabu sana, wikendi ilitakiwa kusiwe na foleni kabisa lakini badala yake ndo foleni balaa, Cheki mji kama Nairobi, wikend magar ni machache mno tena moja moja, Miji ya Bongo wiki nzima ni full huwezi tofautisha jumatatu na juma pili.
 
Mie ndio sielewi kabisa.kwa nini barabara zote mjini dar zimefumuliwa zote na kutengenezwa kwa wakati mmoja? Ingekuwa kwa awamu.
 
Jamani mbona kawaida ss wa mbagala mbona tumeteseka sana kwa kueni wapole wakuu , nanukuu maneno ya mkulu kuwa ukiona foleni sana basi uchumi unakuwa
 
Miji ya Tanzania ni ya ajabu sana, wikendi ilitakiwa kusiwe na foleni kabisa lakini badala yake ndo foleni balaa, Cheki mji kama Nairobi, wikend magar ni machache mno tena moja moja, Miji ya Bongo wiki nzima ni full huwezi tofautisha jumatatu na juma pili.

hii ni nchi ya wasanii hakuna jumamosi wala jumapili.
 
Jamani mbona kawaida ss wa mbagala mbona tumeteseka sana kwa kueni wapole wakuu , nanukuu maneno ya mkulu kuwa ukiona foleni sana basi uchumi unakuwa

hapo ndo tunapopasemea kwa nn ifike kipindi hadi watake izoeleke!???? Kama nchi tunapoteza kiasi gani? ukiondoka mafuta yanayotumika kwenye foleni, muda ambao tungeutumia kwa kuleta maendeleo bado uchovu utaosababishwa na kukaa kwenye gari muda mrefu. Serikali ipo kimya wako bize kutupa mahesabu hewa ya kukukusanya kodi
 
Ndo maana maofisini ufanisi hakuna mtu kaamka sa 10 alfajiri ofisini anafika saa 2. Akifika ofisini hoi ikifika saa 8 mchana anawaza atarudi vipi nyumbani.
 
Of course lazima ufanisi ushuke. Unatarajia ufanisi gani kwa mtu anayeamka saa 10 alfajiri na kulala saa 6 usiku?
 
Kuanzia leo kama ulikua haujui basi mi nakujulisha ukitokea kimara au mbezi chukua barabara ya goba hadi pale mwisho wa hiace kata kulia upite bwaloni kibululu unavuka mto/daraja unapandisha makongo juu chuo cha ardhi hadi mwenge unaenda unakotaka kwenda au goba unanyoosha hadi samaki /tangi bovu unaenda na zako.au mwaogopa mafuta yenu ya vidumu au mwaijua ila amtaki sio wakati wa kulalamika chukua hatuna.
 
mkuu hii barabara ina mawe yaliyosimama kam achupa hasa kutoka mbezi mwisho hadi njia ya kuingia makongo
Kuanzia leo kama ulikua haujui basi mi nakujulisha ukitokea kimara au mbezi chukua barabara ya goba hadi pale mwisho wa hiace kata kulia upite bwaloni kibululu unavuka mto/daraja unapandisha makongo juu chuo cha ardhi hadi mwenge unaenda unakotaka kwenda au goba unanyoosha hadi samaki /tangi bovu unaenda na zako.au mwaogopa mafuta yenu ya vidumu au mwaijua ila amtaki sio wakati wa kulalamika chukua hatuna.
 
Hivi mlikuwa hamna taarifa kuwa waheshimiwa 600 na visindikizi vyao wametumia barabara hii kwenda Dodoma?
 
Back
Top Bottom