Dar: Polisi waua majambazi wawili na kukamata silaha moja

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,366
2,000
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua majambazi wawili na kufanikiwa kukamata silaha moja aina ya Chines Pistol, risasi tatu na maganda manne ya risasi aina ya Chines Pistol.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ametoa wito kwa watanzania kujiepusha na unyang'anyi wa kutumia silaha unaosababisha vifo vya watu wasio na hatia, bali wanatakiwa kufanyakazi za uhalali za kujipatia kipato.

=======

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI NA KUPATIKANA KWA SILAHA MOJA BASTOLA NA RISASI TATU, MAGANDA MANNE YA BASTOLA.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewaua majambazi wawili na kufanikiwa kukamata silaha moja aina ya chines Pistol,risasi tatu na maganda manne ya risasi aina ya Chines Pistol.

Mnamo tarehe 09 Februali 2019 majira ya saa tatu na nusu usiku huko maeneo ya Ukonga kikosi kazi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silahaa kikiwa katika msako wa kuwasaka wahalifu maeneo ya Ukonga kilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Pugu mnadani maeneo ya milimani kuna pikipiki Boxer ambayo haina namba za usajili inazunguka maeneo hayo huku ikiwa na watu wawili waliovalia makoti makubwa.

Ndipo askari wa kikosi kazi hicho wakaanza kuelekea katika eneo hilo na wakiwa njiani kuelekea katika eneo hilo la pugu milimani, ghafla walikutana na pikipiki hiyo maeneo ya Pugu Mnadani na ndipo walipoisimamisha pikipiki hiyo na dereva wa pikipiki hiyo alikaidi amri halali ya Polisi na kuanza kuwarushia risasi askari na ndipo askari wakajibu mapigo ili kujihami na kufanikiwa kuwajeruhi vibaya kwa risasi, majambazi hayo ambayo hayajafahamika majina yao na yanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30.

Askari walipowapekuwa waliwakuta na silaha ndogo bastola aina ya Chines, ikiwa na risasi nne ikiwa imefutwa namba za usajili na pikipiki moja aina ya Boxer nyeusi.

Majambazi hayo yalipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili na kudhibitishwa na daktari kuwa tayari wameshafariki dunia, miili ya marehemu hao imehifadhiwa hospitalini hapo.

LAZARO B. MAMBOSASA-SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
11/02/2019
 

mkia

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
439
500
Siku hizi Polisi hawakamati bali wanaua tu ili wapandishwe vyeo kama JPM alivyoagiza
Huo ni umama. Unataka majambazi yafanywaje ikiwa wanafanya unyang'anyi wa kutumia silaha na wanapambana na polisi. Wewe utakuwa jambazi Tu na mwisho wenu ni chuma tu hakuna namna, mpelekwe mahakamani muhonge mrudi tena uraiani hiyo ni never never never at all

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,776
2,000
Huo ni umama. Unataka majambazi yafanywaje ikiwa wanafanya unyang'anyi wa kutumia silaha na wanapambana na polisi. Wewe utakuwa jambazi Tu na mwisho wenu ni chuma tu hakuna namna, mpelekwe mahakamani muhonge mrudi tena uraiani hiyo ni never never never at all

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mpumbavu
 

TEAM VIBAJAJI

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
1,856
2,000
Mimi kinacho nishangaza ni kitu kimoja,watu ambao hawajahukumiwa kifo na mahakama wanauwawa kiwepesi ili hali kunakundi kubwa magerezani linalo subiria kutekeleza hukumu ya kifo wakiogopa kuwalaza chini,kwanini msiwalaze na hao ili kieleweke?....au walio hukumiwa kifo mkiwalaza chini hawalali🤷🏾‍♂️
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,657
2,000
Hakuna anayetetea majambazi. Lakini pia polisi wasichukue sheria mkokoni na kutoa na kutekeleza hukumu ya kifo kwa mtu yeyote. Tunashuhudia mauaji mengi ya polisi na utetezi wao ni uleule...walipambana na majambazi waliokuwa wakiwarushia risasi askari! Kisha uonyesha silaha zilixokamatwa (tunasikia zingine ni zilezile zilixokwiha onyeshwa huko nyuma). Polisi mnafundishwa jinsi ya kukamata watu hata katika mazingira tata.

Binafsi si muumini wa kutoa uhai wa mtu hata kama ni muarifu. Inaumiza sana ninapoona polisi mkubwa kabisa akitamba na kusifu pokisi wake walivyoua! Mwache Mungu aamue hilo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom