dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua majambazi wawili na kufanikiwa kukamata silaha moja aina ya Chines Pistol, risasi tatu na maganda manne ya risasi aina ya Chines Pistol.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ametoa wito kwa watanzania kujiepusha na unyang'anyi wa kutumia silaha unaosababisha vifo vya watu wasio na hatia, bali wanatakiwa kufanyakazi za uhalali za kujipatia kipato.
=======
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI NA KUPATIKANA KWA SILAHA MOJA BASTOLA NA RISASI TATU, MAGANDA MANNE YA BASTOLA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewaua majambazi wawili na kufanikiwa kukamata silaha moja aina ya chines Pistol,risasi tatu na maganda manne ya risasi aina ya Chines Pistol.
Mnamo tarehe 09 Februali 2019 majira ya saa tatu na nusu usiku huko maeneo ya Ukonga kikosi kazi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silahaa kikiwa katika msako wa kuwasaka wahalifu maeneo ya Ukonga kilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Pugu mnadani maeneo ya milimani kuna pikipiki Boxer ambayo haina namba za usajili inazunguka maeneo hayo huku ikiwa na watu wawili waliovalia makoti makubwa.
Ndipo askari wa kikosi kazi hicho wakaanza kuelekea katika eneo hilo na wakiwa njiani kuelekea katika eneo hilo la pugu milimani, ghafla walikutana na pikipiki hiyo maeneo ya Pugu Mnadani na ndipo walipoisimamisha pikipiki hiyo na dereva wa pikipiki hiyo alikaidi amri halali ya Polisi na kuanza kuwarushia risasi askari na ndipo askari wakajibu mapigo ili kujihami na kufanikiwa kuwajeruhi vibaya kwa risasi, majambazi hayo ambayo hayajafahamika majina yao na yanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30.
Askari walipowapekuwa waliwakuta na silaha ndogo bastola aina ya Chines, ikiwa na risasi nne ikiwa imefutwa namba za usajili na pikipiki moja aina ya Boxer nyeusi.
Majambazi hayo yalipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili na kudhibitishwa na daktari kuwa tayari wameshafariki dunia, miili ya marehemu hao imehifadhiwa hospitalini hapo.
LAZARO B. MAMBOSASA-SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
11/02/2019