comment yako imenipa hope walau kidogo, ila pamoja na hayo makundi yaliyotawala hapo dar kama ulivyoyataja , bado ni % kubwa mno ya wakazi wa hapo ni masikini wa kiwango wa kushindia mlo miwili per day lakini hawajigusi, vichwa viko chini kama kondoo hawaonyeshi nia ya kuchukizwa na umasikini wala hawana hata muda wa kujua chanzo cha umasikini wao, yaani wamemuachia mungu ilimradi kukuche. Watu wa taabu ya namna hii inayotokana na system waliyoiweka kwa ridhaa yao wenyewe wanastahili kuwa front kumpazia sauti mtawala waliomkabithi mamlaka ya kuwatawala na kudai haki yao na kuchochea mabadiliko ya mfumo kujikomboa.Dar wamachinga pekee ndio mmewaacha wanajitokeza peke yao hawana back up ya watu wa kada zingine wakiwa front kwenye kusimamia haki na mabadiliko.Imagine ile kada ya vijana unaopishana nao hapo posta na bahasha za cv's zilizolowa jasho kwa kuzunguka kila kukicha kutafuta ajira hewa, kada hii ingekuwa inanawapa back up hao wamachinga wetu walau hata kuhamasisha na kuwa front kwenye vote ballot walau ili sura za wenye kuhitaji mabadiliko zisiwe zile-zile za wamachinga wa kila siku, Hapo Dar tuna kada kubwa mno ya vijana smart wenye taabu zitokanazo na system na taabu hizo ni kubwa kuliko za wamachinga ila huwa wanajifungia ndani wanaposikia sauti ya mabadiliko ikirindima huko nje na kuwaachia wamachinga pekee wapambane, na kutokana na hulka ya wamachinga obviously inakuwa easy kuwapa wanamabadiliko hawa picha ya wahuni kutokana na nature ya ajira ya wataka mabadiliko mliowaachia jukumu la kuwasaidia kudai haki na mabadiliko.Kenya Mtawala anabehave na anajali watawaliwa kwasabau anajua aki-disturb rights za watawaliwa yeye kama mtawala atapata challenge kubwa kwasababu wanaotoka front kupaza sauti kudai haki na mabadiliko ya system ni watu wa maana: kada za wasomi, wamachinga, wafanyakazi, wasio na ajira n.k.Hakuna mjinga Nairobi, Bunge likifanya maamuzi ya kipuuzi raiya wote bila kujali kada watachonga majeneza ya wabunge na majina yao na kuja nayo nje ya bunge kuwapinga watawala na challenge dhidi ya mtawala inaonekana wazi kwasababu watawaliwa wa kila kada wamejielewa na wamejitokeza kwa pamoja kudai na kusimamia haki inayokiukwa na mtawala na mwisho wa siku mtawala nasurrender na ananyooka.Misri chanzo cha harakati zote za mabadiliko zilianzishwa na Mmachinga aliyejipa ajira hiyo ya umachinga baada ya kumaliza chuo kikuu na kukosa ajira, mmachinga aliyejimwagia petrol na kujiwasha moto hadi kufa kupinga uonevu wa askari wa jiji.Hapa kwetu mtoto anamaliza mpaka masters na anakosa ajira, hajiajiri, ana miaka 40 anakula na kulala kwa wazazi hajigusi hadi kifo chake kitakapomkuta.Shule ni muhimu sana, binafsi kupenda kujisomea ni silaha pekee ya kumuinua mnyonge.Shule ni muhimu sana jamani, shule sio kwa ajili ya kupata ajira , bali kujua wewe ni nani, na unastahili nini na unastahili kufanya nini kupata unachostahili.