Dar - Mlandizi: Utitiri wa Petrol stations

leipzig

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
2,766
1,706
Nimeshtushwa na utitiri wa vituo vya mafuta vilivyo jengwa na kuendelea kujengwa pembezoni mwa barabara kuu iendayo Morogoro na hasa katikati ya Dar Mlandizi,kuna siri gani?

Hapo awali magari mengi yanayoelekea njia hiyo yalikuwa yakijaza mafuta huku mjini Dar lakini nimeshindwa kufahamu kinachoendelea katika utaratibu huu mpya.

Kwa anayefahamu siri iliyopo atujuze!
 
Na wewe fungua kituo chako!hujui kama biashara ya mafuta inalipa?acha wivu wa hivo.
 
Vituo viko wazi tena pembezoni mwa barabara. Hakuna siri hapo, nawe fungua kimoja au kapate ushauri toka kwa wafanya biashara ya mafuta wazoefu wa Lake Oil
 
kwanini Kariakoo kuna utitiri wa maduka ya simu?

kwanini ilala kuna utitiri wa maduka ya spea?

kwanini sinza kuna utitiri wa bar na pub?

kwanini temeke kuna utitiri wa gereji bubu??

haya maswali hukuwaji jiuliza?
 
Nawewe fungua kituo cha mafuta ya kupaka maeneo hayo wala hutakosa wateja
 
Naomba nifunguke,nina wasiwasi na mafuta ya transit ambayo hayajalipiwa kodi badala ya kuvushwa mpakani yanapelekwa katika hivi vituo utitiri na kuuzwa kwa bei nafuu.

Mh. Dr. JPM njoo na huku utumbue majipu serikali inaibiwa kodi.
 
hiyo ndo biashara inayolipa kwa sasa, wananunua pipa kwa 8,000 afu wanauza lita kwa 2,000 hebu fikiria ni faida iliyoje
 
Nimeshtushwa na utitiri wa vituo vya mafuta vilivyo jengwa na kuendelea kujengwa pembezoni mwa barabara kuu iendayo Morogoro na hasa katikati ya Dar Mlandizi,kuna siri gani?

Hapo awali magari mengi yanayoelekea njia hiyo yalikuwa yakijaza mafuta huku mjini Dar lakini nimeshindwa kufahamu kinachoendelea katika utaratibu huu mpya.

Kwa anayefahamu siri iliyopo atujuze!

Hta mim najiulizaga kwanin hcho kipande tajwa kina sheli lukuki cpatag jibu, na hapo ujue kuna nying tu zilivunjwaga enz Magufuli akiwa wazir zilkua zmejengwa ndani ya mita 30
 
Penye mashaka hapakosi jambo...serikali ijaribu kutupia jicho eneo hilo.
 
Kuna some senses kwamba Bararara ya morogoro ndiyo barabara kuu kwa Tanzania. Ina magari mengi yanayosafiri kwenda bara na nje na hivyo vituo vingi vingetumika kujaza mafuta kwenye magari. Lakini uchunguzi unaonesha magari mengi huwa yanajaza mafuta mjini na si kwenye vituo hivi. Sasa kuna siiri gani inayoondelea na vituo hivi?
 
Nimeshtushwa na utitiri wa vituo vya mafuta vilivyo jengwa na kuendelea kujengwa pembezoni mwa barabara kuu iendayo Morogoro na hasa katikati ya Dar Mlandizi,kuna siri gani?

Hapo awali magari mengi yanayoelekea njia hiyo yalikuwa yakijaza mafuta huku mjini Dar lakini nimeshindwa kufahamu kinachoendelea katika utaratibu huu mpya.

Kwa anayefahamu siri iliyopo atujuze!

Jibu lipo kwenye sakata la Lake Oil. Vituo vingi vinapokea mafuta ya tansit na kuyauza hapa Bongo. Maana yake ni kwamba mafuta hayo hayana kodi ya aina yoyote ile. Ni super profit. Ni mtandao kuanzia Uhamiaji kutoa nyaraka feki kwamba gari zimepita mipakani kwenda Zambia, Burundi, Rwanda, DRC na Malawi kumbe ni ujanja tu. Nadhani JPM analijua hilo ndiyo maana kaanza na mkuu wa Uhamiaji.

Taratibu kitaeleweka tu. Kuna vituo vitakufa tu.
 
Mimi naona hayo nayo ni maendeleo na kuonyesha kiasi gani tanzania imepiga hatua kwenye maswala ya usafiri ukijaribu kufuatilia hii miaka ya karibuni watu wamenunua sana vyombo vya moto kwahiyo hivyo vyote vinahitaji mafuta
Na hiyo barabara uliyesema vimefunguliwa vituo vingi vya mafuta hiyo ni international Road yani inaunganisha mwanzo mwa bara la afrika hadi mwisho mwa bara la afrika yani kutoka dar hadi south afrika na hapo kati kuna nchi nyingi sana na hizo nchi nyingi zinategemea bandari ya dar es laaam.
 
Back
Top Bottom