Manispaa ya Sumbawanga imeshamiri, petrol stations kila kona

Manispaa ya Sumbawanga imeshamiri, petrol stations kila kona

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2023
Posts
929
Reaction score
1,310
Wadau nawasalimu,

Nimeamua kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea mkoa wa Rukwa. Baadhi ya maeneo niliyobahatika kuyatembelea ni pamoja na maporomoko ya Kalambo, maporomoko ambayo yapo mpaka na nchi ya Zambia hakika ni kivutio sana ila mkoa wa Rukwa haujayapa uzito mkubwa.

Vile vile nilitembelea bandari ya Kasanga na kuona majengo ya utawala wa mjerumani yanayojulikana kama Bismark. Nilitarajia uongozi wa mkoa wa Rukwa ungeyaboresha kama sehemu ya utalii.

Ziara yangu ikahamia mjini Sumbawanga mji ambao ni makao makuu ya mkoa wa Rukwa pamoja na kujengwa vizuri tatizo kubwa ni ujenzi wa petrol stations kila baada ya mita 50, mita 30, mita 150, mita 250 na nyingine mpaka maeneo ya makazi.

Kuna jengo linabomolewa lipo jirani na nyumba za nhc na ofisi kuu ya ccm mkoa kunajengwa petrol station.

Najiuliza kwanini Serikali inatoa vibali kujenga utitiri wa hivi vituo? Je ukitokea mlipuko nini kitatokea? Je sheria za mipango miji zinasemaje juu ya umbali kutoka petrol station moja mpaka nyingine? Na kwanini petrol stations zijengwe katikati ya makazi ya watu?

Huo ndio mji wa Sumbawanga.

Ziara yangu itaendelea wiki ijayo kutembelea bonde la Rukwa kuliko na ziwa Rukwa.
 
Wadau nawasalimu.

Nimeamua kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea mkoa wa Rukwa. Baadhi ya maeneo niliyobahatika kuyatembelea ni pamoja na maporomoko ya Kalambo, maporomoko ambayo yapo mpaka na nchi ya Zambia hakika ni kivutio sana ila mkoa wa Rukwa haujayapa uzito mkubwa.

Vile vile nilitembelea bandari ya Kasanga na kuona majengo ya utawala wa mjerumani yanayojulikana kama Bismark. Nilitarajia uongozi wa mkoa wa Rukwa ungeyaboresha kama sehemu ya utalii .

Ziara yangu ikahamia mjini Sumbawanga mji ambao ni makao makuu ya mkoa wa Rukwa pamoja na kujengwa vizuri tatizo kubwa ni ujenzi wa petrol stations kila baada ya mita 50, mita 30, mita 150, mita 250 na nyingine mpaka maeneo ya makazi.

Kuna jengo linabomolewa lipo jirani na nyumba za nhc na ofisi kuu ya ccm mkoa kunajengwa petrol station .

Najiuliza kwanini Serikali inatoa vibali kujenga utitiri wa hivi vituo? Je ukitokea mlipuko nini kitatokea? Je sheria za mipango miji zinasemaje juu ya umbali kutoka petrol station moja mpaka nyingine? Na kwanini petrol stations zijengwe katikati ya makazi ya watu?

Huo ndio mji wa Sumbawanga

Ziara yangu itaendelea wiki ijayo kutembelea bonde la Rukwa kuliko na ziwa Rukwa
Gas station sio kibanda cha nyanya,vibali vinatolewa kwa kuangalia na suala la dharura pia
Nilidhani unakuja na analysis ya kitalaamu apa kumbe ni wivu unakusumbua
Izo filling station umepita morogoro road ukazihesabu sindio utadata kabisa

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Utalihi bila picha/video clip sawa na takataka tu dunia ya ss .
 
Back
Top Bottom