Dar: Mfanyabiashara Mohammed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Watekaji inasemekana walikuwa na silaha kali hata kama alikuwa na body guard asingeweza kuzuia. Hii kulingana na matangazo ya redio yanayotangazwa na Charles Kiswanta wa Zenj.
Tycoon kama MO anakuwa na ulinzi binafsi. Tena wa makomandoo kabisa, siku zote mtekaji akishazingilwa haijalishi ana kifaru au SMG lazima ata surrender tu. Maana inayomuua mtu sio ile siraha, la hasha ni risasi iliyondani ya siraha, tena yenye ukubwa wa kipenyo cha sm 5!!
 
Duh!Watu wasioujulikana hao bila shaka!

Hii nchi sasa!!

Walitekwa na kupotea watu wa kawaida, tukaona ni mambo madogo.Leo wanatekwa matajjri na watu maarufu labda sasa ndio tutashituka.

Nakumbuka pia yaliompata Lissu na mfanyabiashara wa Tarime bwana Zakaria.

Wacha tusubiri tuone nini kinaendelea tutapata picha kamili.

Kwa sasa wanaweza kuwa wanapima upepo.Pressure ikiwa kubwa,wanaweza kumwachia ikiwa mpaka sasa bado yuko salama.

Hii update kuwa katekwa na wazungu,inanipa maswali mengi sana na mojawapo ni wazungu gani hao wa kumteka mtu tajiri kama huyo tena wakiwa katika nchi ya watu?

Wanajiamini nini?
Kwa hiyo nini kifanyike
 
Hamna kuishi na watu ukishakuwa bilionea wa kidunia huwezi kuishi kama raia wa kawaida watu wanaoweza kujudhuru ni wengi.

Ww unadhani unaweza kukutana na Abrahamovic anatembea bila hata mlinzi?!eti anaenda public gym ni uzembe wa hali ya juu hamna bilionea wa kidunia ambaye anaishi kama kuku wa kienyeji eti aende public gym bila ulinzi.


Huko kwny viwanja vya mpira kwenye kumetengwa maalum kwa watu muhimu labda ww ndio hujui
Mo amejiteka anatafuta kick.
 
Yamezidi awamu hii lakini si kuanza awamu hii. Ulimboka alitekwa awamu hii? Hivi vitu tuvilaani kwa nguvu zote. Ombi langu kwa Mungu unaweza usilielewe lakini si lazima nieleweke. Serikali ijue tukio hili linaenda kukamilisha dhana iliyopo kwa utimilifu wake kama wasipolibeba kiweledi na kuheshimu misingi ya utu na ustawi wetu.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya utekaji wa miaka ya nyuma na huu wa sasa! Utekaji wa miaka ya nyuma ni ule wa kutoa ujumbe kwamba "serikali haichezewi." Ulikuwa ni utekaji wa kutia watu adabu na kisha kuwaacha wakaendelee na maisha yao!

Kinyume chake, utekaji huu wa sasa, ukisalimika kwa kuliona jua la siku zinazofuatia, basi unatakiwa ukapike sadaka! Huu ni utekaji unaokusudia kuwapoteza kabisa victims.
 
Ni propaganda ambazo hazina maana kama atakua hana ushahidi wa kutosha ..maana hata albino akivaa maski ukitizama na kumtofautisha kwa rangi ya ngozi tu unaweza kuishia kusema ni wazungu, pia watekaji wanaweza wakavaa fake skin kuwapoteza maboya polisi na mashahidi
Hili nalo neno mweh!
 
Tycoon kama MO anakuwa na ulinzi binafsi. Tena wa makomandoo kabisa, siku zote mtekaji akishazingilwa haijalishi ana kifaru au SMG lazima ata surrender tu. Maana inayomuua mtu sio ile siraha, la hasha ni risasi iliyondani ya siraha, tena yenye ukubwa wa kipenyo cha sm 5!!
Kule Tarime yule mfanyabiashara Peter Zacharia yeye hakuwakawiza walipojipendekeza aliwatwanga Risasi ndiyo njia sahihi ya kujikinga na wasiojulikana
 
Hao watu wasiojulikana ni hakina nani wasio na kifani cha kuwa adharani,?

Hao watu wasiojulikana huwa wanaishi angani, baharini mpaka kuwepo utata juu yao?

Zibaki kuwa ndoto endapo wakimdhuru wanayo majibu ya kutoa
 
Waliofunika uso wamewajuaje kama ni wazungu? Wahindi, wachina au warusi maana hao ndo wanaujuzi wa kupoteza watu chini ya Putin. Labda wakwetu wamekwenda kozi huko.
Katika ukusanyaji wa ushahid/taarifa it is scientific procedure kuanzia kuanza kuchunguza na ni lazima wakusanye taarifa zile zilizoonekana katika eneo la tukio hayo mengine yatakuja tu kama ni wahindi au wachina ila kwa sasa walionekana pale ni whiteman so acha vitengo vya instigation wafanye kazi yao waza kisomi
 
Kweli mkuu...

Unajua nchi yetu ilipofikia ni katikati ya maendeleo na machafuko.

Watu wamekua wanakumbatia sana siasa kuliko uzalendo wa nchi yao.

Tunachokitafuta tutakipata...muda utasema.
Kwa akili zangu nilikuwa najua watu waliofikia level kama hiyo kuna mambo mengine ambayo hawashindwi kuyapata kuwa nayo katika mazingira yao yanayowazunguka kwa usalama zaidi ...mfano kuwa na gym binafsi kwa tajiri kama huyu nahisi ingelikuwa poa

Ila kuna kipindi alikuwa anapost mambo ya madeni maden sijui tuunge doti ?
 
Back
Top Bottom