DAR: Majambazi wavamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia, wapora fedha na vifaa vya kuendeshea misa

kupora fedha...
Tutaelewa

na vifaa vya kuendeshea misa.
Hii hatuelewi, ila bangi na madawa ya kulevya waweza fanya lolote lile..
Pole kanisa katoliki...
Ndio kuna vifaa vya kuendeshea misa, mfano vikombe vya kuwekea mwili wa kristo na damu yake huwa ni vya thamani kiasi kwamba wakienda kwa masonara wanayeyusha na kupata bidhaa zingine
 
Majambazi wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho na kupora fedha na vifaa vya kuendeshea misa.

Paroko wa parokia hiyo, Sunil Kishor amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Chanzo: Mwananchi
Itakua sio majambazi hao. Kuna namna hapo
 
Hongera Mkuu kwa kufika mbinguni na kufunguliwa geti
hiyo hongera ipe bibilia mkuu sio mimi. Ufunuo 21
"mji wenye mageti 12"
hapo nimetoa ushauri tu, hata kanisani kwangu niliwapa ushauri wahusika watafute safe, au waboreshe maana kuna vitu vya thamani ambayo vinatuzwa kizembe lkn sijaona initiative yoyote, kesho vikiibiwa wataanza kumlilia Mungu tena.

Mungu hawezi kutufanyia vile ambavyo ameshatupa uwezo tayari wa kuvifanya.
Hatuzuii kbisa bali tunapunguza uwezekano. Ndio maana nimetoa pole kwa tukio.
 
Khaa..... KUMBE MISA INAENDESHWA NA VIFAA..... inabidi wanunue vingine haraka sana ili misa iendeshwe.
 
kupora fedha...
Tutaelewa

na vifaa vya kuendeshea misa.
Hii hatuelewi, ila bangi na madawa ya kulevya waweza fanya lolote lile..
Pole kanisa katoliki...
Huwa wanaiba wakidhani zile chetezo n.k ni pure gold.
Niliwahi kusikia, sijui kama kweli au uongo, hostia zilizobarikiwa zinafutwa sana na waabudu shetani; wana uanua moja si chini ya 4m
 
Ok. Hata kama. Lakini njia za kuifikia benki siku hizi nyingi sana. Walishindwaje? Au katuma watu yeye mwenyewe paroko. Halafu ni Dar na panajulikana kwa uhalifu halafu unahifadhi fedha kanisani. Kama wanapora benki vipi washindwe kanisani kunakolindwa kwa imani kama si rungu?
Mkuu huwa kuna vijisadaka vya ibada asubuhi za kila siku ambazo haziwezi kukushawishi kuzipeleka benki . Ni pesa unakuta haifiki hata laki . Sasa sijajua wameiba sadaka za lini , lakini hawawezi kukutana na sadaka ya jpil hata kwa bahati mbaya . Ngoja tusikie habari kamili kwanza .
 
kama ni petty cash kwa ajili ya matumizi madogo madogo unapeleka benki?
Kumbe pettycash hata ikiibiwa si tatizo? Kanisa laweza kulipa kwa namna tofauti. Cheki au mifumo ya Mpesa, halopesa, tigopesa nk. Lakini kuhifadhi hela kanisani ni ujinga na matumizi mabaya ya rasilimali watu. Lazima mtataka polisi wafuatilie. Kwa uzembe wenu tuache kazi za maana tufanye hii. Hata uswisi benki makanisa yanalindwa. Acheni uzembe RC
 
Sina uhakika kama tukio hili lina uhusiano na waraka wa TEC au ibada ya Pasaka pale Posta ya zamani Dar .
 
Ndio kuna vifaa vya kuendeshea misa, mfano vikombe vya kuwekea mwili wa kristo na damu yake huwa ni vya thamani kiasi kwamba wakienda kwa masonara wanayeyusha na kupata bidhaa zingine
Kumbe inafahamika vya thamani halafu vinaachwa bila ulinzi madhubuti.
 
Back
Top Bottom