Dar, Kisutu: Kesi namba 112/2018 inayowakabili Viongozi Wakuu wa CHADEMA, inaendelea leo

Mahakama ikijilidhisha pasina shaka,adhabu ya mbwa koko itolewe.
najuua una akili ndogo kama mtto mdogo lakini nikuulize msingi wa case ni upi hapo? kwamba mkusanyiko usio halali ni upi wakati katiba inasema kila mtu anaouhuru wa kwenda popote bila kuvunja sheria za nchi. na kwamba mambo sasa alishakiri aliyefyatua risasi ni polisi na kwamba jamhuri iligharamia maziko. ni vielelezo tosha kuwa hayo unayotaka wewe hayawezekani. kkwenye kesi ya zombe na wenzake zidi ya jamhuri aliyefyatua risasi ndgu mageni ndio ananyea debe kwann hawajafungwa wote kama unadhani ni rahisi.
 
Vyama vya siasa havina dini usivihusishe na Mungu
Chama kisicho na dini ni ccm pekee , huwa nashangaa pale Mwenyekiti wake anapotaka kuombewa , au anamaanisha aombewe kwa mizimu ?

Chadema Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu
 
Ni Nani aliyemuua Akwilina?
Kwa kuwa hakuna polisi aliyefunguliwa mashtaka kuna haja ya kesi kweli? C wawafunge tu tujue moja?
Kesi namba 112/2018 inayowakabili Viongozi Wakuu wa CHADEMA. M/kiti wa Chama Freeman Mbowe (Mb) KM Dkt Mashinji, NKMB Mnyika (Mb), NKMZ Salum Mwalim, Mkt wa BAWACHA Taifa Halima Mdee (Mb), John Heche (Mb), Ester Matiko (Mb) na Peter Msigwa (Mb), inaendelea leo kuanzia saa 3 asubuhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ni katika kesi inayowakabili katika mahakama ya Kisutu wakituhumiwa kuandamana kinyume cha sheria.

=====

Kesi ya kula njama na kufanya mikusanyiko isiyokuwa ya halali inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe imeanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakati kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikianza kusikilizwa, mshtakiwa wa saba, Halima Mdee na mshtakiwa wa tisa Ester Bulaya hawapo mahakamani.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala ameieleza Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa sababu ya washtakiwa hao kutokuwapo mahakamani imetokana na usafiri waliokuwa wanatumia kutoka bungeni mjini Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kuwa na tatizo na kusababisha wachelewe kufika.

Mbali na Mbowe ,washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa; naibu makatibu wakuu Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara) ambaye pia ni mbunge wa Kibamba.

Wengine, mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko; Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kufanya mkusanyiko usio halali ama

maandamano yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

Chanzo: Mwananchi

Habari zaidi, soma=>Kutoka Kisutu: Mbowe na viongozi wengine sita wa CHADEMA Wapata dhamana
 
Back
Top Bottom