Dar, Kisutu: Kesi namba 112/2018 inayowakabili Viongozi Wakuu wa CHADEMA, inaendelea leo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,759
Kesi namba 112/2018 inayowakabili Viongozi Wakuu wa CHADEMA. M/kiti wa Chama Freeman Mbowe (Mb) KM Dkt Mashinji, NKMB Mnyika (Mb), NKMZ Salum Mwalim, Mkt wa BAWACHA Taifa Halima Mdee (Mb), John Heche (Mb), Ester Matiko (Mb) na Peter Msigwa (Mb), inaendelea leo kuanzia saa 3 asubuhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ni katika kesi inayowakabili katika mahakama ya Kisutu wakituhumiwa kuandamana kinyume cha sheria.

=====

Kesi ya kula njama na kufanya mikusanyiko isiyokuwa ya halali inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe imeanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakati kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikianza kusikilizwa, mshtakiwa wa saba, Halima Mdee na mshtakiwa wa tisa Ester Bulaya hawapo mahakamani.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala ameieleza Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa sababu ya washtakiwa hao kutokuwapo mahakamani imetokana na usafiri waliokuwa wanatumia kutoka bungeni mjini Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kuwa na tatizo na kusababisha wachelewe kufika.

Mbali na Mbowe ,washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa; naibu makatibu wakuu Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara) ambaye pia ni mbunge wa Kibamba.

Wengine, mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko; Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kufanya mkusanyiko usio halali ama

maandamano yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

Chanzo: Mwananchi

Habari zaidi, soma=>Kutoka Kisutu: Mbowe na viongozi wengine sita wa CHADEMA Wapata dhamana


====

UPDATES

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana huu imetupilia mbali ombi la upande wa utetezi la kutaka kesi inayowakabili viongozi Tisa wa ngazi za juu CHADEMA kupelekwa Mahakama kuu ambapo sasa usikilizaji wa awali utaanza rasmi kesho saa nane mchana.
 
Mwenye kumbukumbu anisaidie Kamanda Mambo sasa alitamka nani wanashikiliwa kwa tuhuma kifo Akwilina!? Je walifikishwa katika vyombo vya sheria!?Familia yake na Watanzania wengi wapenda amani wanachukulia vipi hili!?Mimi najisikia vibaya.
 
Melo hawezi kudeal na sisimizi kama wewe, acha kujipaisha na kujipa umuhimu usiokuanao.

Aliyelift ban ni moderator huyohuyo aliyekupiga ban zuzu wewe.

Hahahahaha mkuu umempa stahiki yake huyu mjinga safi sana
 
Mwenye kumbukumbu anisaidie Kamanda Mambo sasa alitamka nani wanashikiliwa kwa tuhuma kifo Akwilina!? Je walifikishwa katika vyombo vya sheria!?Familia yake na Watanzania wengi wapenda amani wanachukulia vipi hili!?Mimi najisikia vibaya.
Mimi nimepoteza kumbukumbu nipo hapa shambani nazitafuta
 
Yaani yajayo yanafurahisha, hii ni kweli maana tulizoea mtu kuzeeka in tendo la taratibu sana na lina chukua muda kuona mabadiliko hata miaka 20.
Lakini kwa Mh. yeye kwa siku 7 tu amekimbiza sana.
images

images

Unawaza kuona mahandsome ktk pics ya pa1

sege.jpg

images
 
Kesi ya kula njama na kufanya mikusanyiko isiyokuwa ya halali, inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, imeanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

mbowe.jpg
 
Sheria ifuate mkondo wake,kama hawana hatia waachiwe,wakipatikana na hatia ,hakuna kuangalia mtu usoni,sheria wametunga wenyewe bungeni
 
Back
Top Bottom