dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,474
TAARIFA YA TUKIO KUBWA KWA KIREFU
KGD/IR/4422/2019
KOSA MAUAJI
MTOA TAARIFA NI SP THOBIAS WALELO MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA KIGAMBONI
Anaeleza kuwa mnamo tarehe 15.07.2019 majira ya saa 0800hrs huko Gezaulole kata ya Somangila Wilaya ya Kigamboni jiji la Dar Es Salaam nyumbani kwake Khamis Said Luongo, 38yrs, Makonde, Mfanyabiashara , mkazi wa Gezaulole. Anaeleza alimpinga na kumuua mke wake aitwaye Naomi Orest Marijani, 36yrs, Mpare, mfanyabiashara na mkazi wa Gezaulole.
Mara baada ya mauaji hayo Khamis Said Luongo anaeleza kwamba alichukua mwili wa mke wake na kuuweka mwili kwenye shimo alilochimba kwenye banda lake la kufugia kuku kisha aliweka mkaa gunia mbili na mafuta ya taa kisha akawasha moto ulio waka muda mrefu na mwili wote kuteketea kuwa majivu.
Kisha alichua majivu hayo akaweka kwenye mfuko na kubeba kwa kutumia gari lake lenye no T 206 CEJ aina ya Subaru Forester rangi nyeusi na kupereka kwenye shamba lake lililoko kijiji cha mlogolo kata ya vikindu wilaya ya Mkulanga Mkoa wa Pwani.
Alichimba shimo kwenye shamba lake kisha kuweka hayo majivu na kufukia na akapanda mgomba juu yake. Kisha Khamis Said Luongo alikaa nyumbani kwake akisema mke wake ametoroka nyumbani.
Tarehe 19.05.2019 alifugua taarifa ya mke wake kutoroka nyumbani na kupewa RB ya kituo kidogo cha Mjimwema MJ/RB/234/2019 yahusika.
Kisha kuwajulisha ndugu jamaa na marafiki zake kuwa mke wake ametoroka nyumbani.
Tarehe 12.06.2019 alifungua jalada KGD/IR/3617/2019 kosa kuterekeza mtoto.
Akimtuhumu mke wake kuwa ametelekeza mtoto aitwaye Gradous Khamis mwenye umri wa miaka 6.
Tarehe 13.06.2019 ndugu wa Naomi Orest Marijani walitoa malalamiko yao ya kupotea kwa ndugu yao kukafunguliwa jalada la uchuguzi Temeke/CID/PE/69/2019 yahusika.
Upelelezi uliedelea Khamis Said Luongo akiwa anaenda kulipoti ofisi ya RCO Temeke.
Hadi tarehe 15.07.2019 Khamis Said Luongo alizuiliwa na mahojiano ya kina kufanyika ndipo akaamua kusema ukweli kuwa alimuua mke wake na tarehe 16.07.2019 aliongoza timu ya makachelo kutoka kanda ofisi ya ZCO ofisi ya RCO Temeke wataalam kutoka PHQ daktari iliyokuwa inaongozwa na ASP Msisiri OCS Kigamboni walifanikiwa kupata mabaki ya mwili yamechukuliwa kwenda kanda kwa ajili ya uchuguzi zaidi.
Chazo cha mauaji ni wivu wa kimapenzi.
Tukio limekaguliwa na SP. Thobias Walelo OC CID Kigamboni akishirikiana na makachelo.
Upelelezi unaendelea nitaendelea kukujulisha maendeleo.
Zaidi, soma.....
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania linamshikilia Khamis Luwonga maarufu Meshack mkazi wa Kigamboni kwa tuhuma za kumuua mkewe, Naomi Marijani.
Luwonga anadaiwa aliuchoma moto mwili wa mkewe.
Mkuu wa Upepelezi wa kanda hiyo, Camillius Wambura akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Julai 17, 2019 amesema wanamshikilia kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.
Amesema pamoja na kumhoji polisi wamekwenda katika maeneo ambayo ameyataja kufanya mauaji hayo kwa ajili ya kupata uthibitisho.
“Huyu bwana tunaye tunaendelea kumhoji na askari wameshakwenda katika maeneo aliyoyataja, wamechukua majivu kwa ajili ya vipimo vya DNA kuona kama kweli yanaendana na huyo mama,” amesema
Joseph Hatia, shemeji yake Naomi amedai kumekuwa na taarifa kuwa Naomi na mumewe hawakuwa na maelewano mazuri hadi siku anatoweka.
Amesema kwa taarifa walizozipata Meshack ameeleza kwamba siku ya tukio alirudi nyumbani na kumkuta mkewe lakini waligombana.
“Wakiwa wanagombana na kusukumana amedai kwamba Naomi alidondoka na kujigonga kichwani, alivyoona hivyo akamburuza hadi nje na kuchimba shimo akamtumbukiza na kuchoma moto.”
Hatia amesema kwa sasa familia inasubiri taarifa rasmi kutoka kwa polisi ambao wanaendelea kumshikilia Luwonga.
Naomi alitoweka nyumbani kwake Mei 15, 2019 na familia yake ilitoa taarifa polisi katika kituo cha Chang’ombe baada ya mumewe kuwajulisha siku nne tangu atoweke.