Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,810
- 11,981
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LINAWASHIKILIA WATU 92 KWA TUHUMA MBALIMBALI ZA KIHALIFU.
JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LINAENDELEA NA JUKUMU LA KUIMAIRISHA ULINZI NA USALAMA WA RAIA NA MALIZAO NA, KUANZIA TAREHE 1/1/2022 HADI 19/1/2022 KUMEKUWA NA MSAKO MKALI DHIDI YA WATU WANAOPANGA NJAMA ZA KUFANYA UHALI
LAKINI PIA KUWAKAMATA WALE AMBAO
WAMEKWISHAFANYA UHALIFU. WATU HAO WAMEHUSISHWA NA VITENDO VYA UNYAN`GANYI, WIZI WA MAGARI, PIKPIKI, WIZI WA PESA, NA BIASHARA YA KUSAFIRISHA, KUUZA NA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA; -
TAREHE 19/01/2022 MAJIRA YA SAA TANO USIKU MAENEO YA TOANGOMA MASAKI ALIKAMATWA MTUHUMIWA NICAS PROSPER MUSHI, MWANAUME MIAKA 23, MCHAGA MKAZI WA TOANGOMA MASAKI AKIWA NA MALI ZA WIZI ZENYE THAMANI YA MILIONI 36,645,400/= ZA KITANZANIA.
MALI HIZO NI; -
SIMU (smart phones) AINA MBALIMBALI ZENYE THAMANI YA TSHS 14,070,000/=
PESA TASLIMU ZA KITANZANIA 9,135,500.
PLAY SATATION 5 ZENYE THAMANI YA TSHS 3,000,000/=
MABEGI 19 YENYE THAMANI YA TSHS 2,040,000/=
MODEM YENYE THAMANI YA TSHS 150,000/=
BLUETOOTH DIVICE MOJA YENYE THAMANI YA TSHS 140,000/=
POWE BANK MOJA YENYE THAMANI YA TSHS 130,000/=
FULL SCREEN PROTECTOR YENYE THAMANI YA TSHS 250,000/=
KAVA ZA SIMU ZA MKONONI 35 YENYE THAMANI YA TSHS 600,000/=
SAA ZA MIKONONI 35 YENYE THAMANI YA TSHS 455,000/=
CV GAME 5 YENYE THAMANI YA TSHS 600,000/=
CONTROLER 2 PLAY SATATION 5 ZENYE THAMANI YA TSHS 500,000/=
EXATION 2 PLAY SATATION 5 ZENYE THAMANI YA TSHS150,000/=
SPIKA BULTHER YENYE THAMANI YA TSHS 210,000/=
PLAY SATATION 5
MTUHUMIWA ALIIIBA VITU HIVYO KUTOKA KWA ASIFU SAJADI AMBAYE AMEKWISHAVITAMBUA
WATUHUMIWA 15 WANAUME WANASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI ZIFUATAZO; -
GARI NDOGO MOJA AINA YA CARINA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 325 CYB
TV 2 INCH 32 STAR X NA 42 SAMSANG
MITUNGI 2 YA GESI KG 14
GENERATOR 1
KING`AMUZI CHA DSTV 1
SABUFA 1
SIMU YA ITEL (smart) 1
BOX 3 ZA BRENDER
BOX MBILI ZA RICE COOKER
PIKIPIKI NANE MC 869 AKM AINA YA HON LG NA MC 233 CXX AINA YA BOXER RANGI NYEUSI NA MC 167 CNV AINA YA BOXER NA MC 745 CWL AINA YA TVS NA MC 156 CQD AINA YA TVS, MC 418 CKM AINA YA TVS, MC 593 CRT AINA YA TVS NA MC 219 CTS AINA YA TVS.
KATIKA HATUA NYINGINE JESHI LINAWASHIKILIA WATU 74
WA KIUME NA 2 WAKIKE KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA KUSAFIRISHA, KUUZA NA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA KAMA. HEROINE KETE 18, BHANGI KG 23.51, KETE 1709 PULI 93, MISOKOTO 2,221 NA MIRUNGI KGM 40 ZILIKAMATWA.
JESHI LINAMSHIKILIA PIA MTUHUMIWA AITWAYE
RENATUS GREGORY MUABHI MIAKA 53, MKAZI WA UBUNGO, KWA TUHUMA ZA KIJIFANYA AFISA WA USALAMA WA TAIFA KWA LENGO LA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA
UDANGANYIFU (KUTAPELI) MAENEO MBALIMBALI ZIKIWEMO OFISI ZA SERIKALI
JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LINATOA RAI KWA WATU WANAOENDELEA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA KIHALIFU KUACHA MARA MOJA KWANI WAKIFANYA WATAJIKUTA KATIKA MSUGUANO MKALI NA MIFUMO YA SHERIA.
Muliro JUMANNE MULIRO– ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.