Dar ipi iko vizuri kuliko nyingine?

Dar ipi iko vizuri kuliko nyingine?

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,243
Dar ni mji mkubwa sana kiasi kwamba wengi wetu hadi tunakufa sehemu nyingine za mji huu tutazisikia redioni. Kutokana na ukubwa huo Dar haifanani hata kidogo. hebu tupe tathimini yako wapi wamewazidi wapi na wamewazidi kwenye nini?


  1. Wapi ni wakali wa kushabikia maisha ya ulaya wakati mfukoni hawana kitu na elimu yao ni ya kuungaunga?
  2. Kinadada poa wamefurika wapi na ni wapi watu hao wanaonekana ni wa kawaida?
  3. Klabu za usiku za ukweli ziko wapi na ipi ni kali kuliko nyenzie?
  4. Eneo lipi ni hatari kuishi na hatari yake ni ipi?
  5. Wakali wa kuuza Mapupu, utumbo wa kuku na miguu yake, maharage ya kupima, na samaki wa kukaanga wapi wanapatikana?
  6. Shule bomba za Msingi na sekondari kwa ubora wa majengo na ufundishaji unaweza kuzitaja?
  7. Wapi shida ya maji ni ya kawaida kama vile kuchomoza na kuzama kwa jua?
  8. Watoto wa ukweli wanatoka kwa wingi wapi?
  9. Akitaka ajue shida ya usafiri mtu akaishi maeneo gani ya Dar?
  10. Wapi wamekubuhu kwa kutupa hovyo hovyo takataka?
  11. Eneo gani la Dar limepimwa vizuri na lipi ipo shaghalabaghala hadi inatisha?
  12. Uswazi ya kweli dar iko wapi.

Dar itabaki kuwa Dah!
 
Nenda dar kafanye Research! Alafu toa ripoti yako!! Na maswali utakuwa umeyapatia majibu!,
 
Back
Top Bottom