Dar inaongoza kwa ngono, rushwa

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
na Lucy Ngowi

MBUNGE wa Viti Maalum, Janeth Massaburi (CCM), amebainisha kuwa mkoa wa Dar es Salaam, unaongoza kwa rushwa ya ngono hasa kipindi cha uchaguzi au mtu anapotaka uongozi.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es salaam kwenye semina ya ukimwi iliyoendeshwa na taasisi ya Engender Health kwa wabunge wa Kamati ya Bunge inayohusika na masuala ya ukimwi.
Massaburi alisema, mtu anayetaka nafasi ya kuongoza kwenye uchaguzi, kampuni binafsi na serikalini, ngono imekuwa ni sehemu ya kigezo cha kupata nafasi hizo.
“Umaskini unasababisha rushwa ya ngono, mtu anapotaka nafasi yoyote ya kuongoza ili ajulikane, iwe ni kwenye kampuni binafsi, serikalini au katika kipindi cha uchaguzi anatakiwa atoe rushwa ya ngono.
“Wasiwasi wangu watu wanafanya hivyo ili kupata cheo, hasa kwenye jimbo langu la Dar es Salaam ambalo nimeona hali hiyo ikijitokeza mara kwa mara,” alisema Massaburi.
Aliongeza kuwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamekuwa wakijidanganya kuwa wana uelewa mkubwa wa ugonjwa huo wakati ukweli si huo.
Alishauri Engender Health iwatumie wabunge wa majimbo, viti maalumu na madiwani ili waweze kuwafikia wananchi kwa urahisi na kuwaelewesha kuhusu athari za ugonjwa wa ukimwi.
Naye mbunge wa Jimbo la Bukene, Teddy Kasella-Bantu (CCM), alisema katika jimbo lake ngoma na ulinzi wa sungusungu vinachangia kuwepo kwa ongezeko la ukimwi kwa kuwa wananchi hawana elimu ya kutosha.
“Katika jimbo langu kuna kitu kama ngoma, ambazo zinakuwepo kwa wingi sana. Sasa baada ya ngoma hiyo kinachofuata ni maambukizi ya ukimwi. Pia kwenye makundi yoyote hasa ya sungusungu maambukizo haya yanakuwepo,” alisema.
Aliongeza kuwa katika jimbo lake, hakuna suala la uzazi wa mpango na hivyo wananchi hao wanahitaji kupata zaidi elimu kuhusu suala hilo.
Mbunge wa Konde, Kaskazini- Pemba (CUF), Dk. Ali Tarab Ali, alisema kuwa katika jimbo lake kuna tatizo kubwa la vifo vya kina mama na watoto kutokana na ukosefu wa vituo vya afya.
Awali, Naibu Mkurugenzi wa Engender Health, Dk. Dunstan Bishanga, alisema kuwa baadhi ya tabia hatarishi zinazofanywa na wanaume zinachangia kuwepo kwa virusi vya ukimwi, ambapo athari kubwa zinawapata wanawake. Alisema wabunge wanatakiwa kuwa wakala wa mabadiliko katika masuala yahusuyo ukimwi na maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto.

Source
http://freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=14323
 
Hamna jipya hapo!


Ya kweli hayo? Mimi nafikiri jipya lipo hapa. Aliyetoa hiyo kauli ni mwanamke na nina imani tayari aliishakutana na masuala haya ndio maana akasema. Nakifikiri tungeitumia nafasi hii kusikia vile vile kutoka kwa wanawake wengine walio humu JF kama hayo yaliyosemwa ni ya kweli au hapana kuliko kusema hakuna jipya hapa.

Tiba
 
mbona kaongelea uchaguzi

ATUELEZE MAMBO YOTE WANAYOFANYA WABUNGE WAKIWA ""DODOMA""!!!!

DOM MAMA JANE DOM KUNA UCHAGUZI IWEJE LEO UMEONA HAYO KWENYE UCHAGUZI WAKATI WAH WANA DO BILA UCHAGUZI
 
Takukuru wahusishwe na kuhakikisha mtindo huu mchafu unakomeshwa!!!

Tiba

Weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
kunguru wapotea!!!!!!!!!!!!!kunguru wapotea!!!!!!!!!...waka.......
 
Back
Top Bottom