Mkakati wa Ukawa kusimamisha mgombea mmoja kila jimbo la Uchaguzi ni akili kubwa.
Tathmini kwa Mkoa wa Dar es salaam unaipa Ukawa nafasi kubwa zaidi ya Ushindi kulinganisha na CCM. Ukawa itanyakua majimbo 6 kati ya nane. Majimbo ambayo kwa zaidi ya asilimia 90% yatatua Ukawa ni pamoja na Ubungo,Kawe, Segerea,Kigamboni, Ukonga na Temeke. Mfano Jimbo la Ubungo kwa Uchaguzi wa 2010 CUF ilipata kura 12,000 nyingi zikitokea ngome za manzese. Segerea CUF wananguvu sana eneo la Buguruni ambapo ndipo kuna voters wengi zaidi. Temeke CUF+CDM kwa pamoja wana nguvu kuliko CCM. Kawe kutakuwa hakuna ushindani kwa kuwa kura za Mbatia zinakwenda Ukawa. Hali ya Ukonga na Kigamboni inafanana na Temeke.Hakuna jinsi ambayo CCM inachukua majimbo hayo.