Dar es salaam: Tandale kwa mtogole na jaramba la sasambua sasambua

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165


Niliamka alfajiri na mapema, ilikuwa ni kama saa 10:30, na kujiandaa, pamoja na kuandaa uji wa mgonjwa. Nilikuwa nauguliwa nashangazi yangu na alikuwa amelazwa Hospitalini Muhimbili akisumbuliwa na Presha pamoja na kisukari.

Baada ya kujiandaa majira ya saa 11:00 nilitoka na kuelekea kituoni cha basi pale Magomeni Makanya, nilipofika pale nilikuta abiria kadhaa na nikajiunga nao kusubiri daladala, haikuchukua muda daladala moja aina ya Toyota Coster likafika na abiria wote tuliokuwa pale kituoni tukapanda, nilipata siti ya mbele karibu na dereva nikakaa na abiria wote walipoingia tuliondoka. Daladala letu lilikuwa likienda huku likipakia abiria wengine njiani.

Tulipofika maeneo ya Tandale kwa Mtogole basi letu likasimama ili kupakia abiria, na waliingia abiria saba, wanawake watatu waliokuwa wamevaa mahijabu yaliyofunika nyuso zao kama maninja na wanaume wanne waliokuwa wamevaa kanzu.

Walipoingia wote kabla basi halijaondoka, mwanamke mmoja miongoni mwa abiria wale alikwenda moja kwa moja kwa dereva na kuchomoa panga kutoka kibindoni na kumuwekea dereva shingoni na kisha kuzima gari na kuchukua funguo, wakati huo huo miongoni mwa wale abiria mwenye kanzu alimuamuru kondakta akae kwenye kiti huku akiwa amemshikia panga vile vile, wale abiria waliokuwa na mahijabu, tuliodhani kuwa ni wanawake, kumbe walikuwa ni wanaume. Walitandika kitambaa cheupe na kutuamuru abiria wote tuliokuwa ndani ya lile daladala kila mmoja aweke kila alicho nacho pale katika kitambaa akianza na simu. Walikuwa wakiimba ule wimbo maarufu huku Pwani unaotumika wakati wa kumtunza bi harusi kabla ya kuolewa uitwao sasambu sasambu, wakitaka kila mtu asasambue alicho nacho na kukiweka katika kile kitambaa.

Baada ya kuona kama vile tunachelewa walianza kutupiga kwa ubapa wa upanga na kutisha kuwa atakayekuwa mbishi au kujitia ujanja watamuua kwani hawana cha kupoteza, wanawake wote tulinyang'anywa mikoba yetu na cha kushangaza hata kile kikapu klichokuwa na uji wa mgonjwa walikibeba.

Kuna mzee mmoja hakuwa na simu na hiyo ilimgharimu, kwani walimpiga kwa ubapa wa upanga mpaka akajifanya amezirai ndio wakamuacha, wakati zoezi hilo likiendelea vibaka wengine walikuwa nje na kazi yao ilikuwa ni kutishia daladala nyingine zilizotaka kusimama katika eneo lile zisisimame.

Ilikuwa kila daladala likitaka kusimama wanapiga mapanga kwenye bodi ya daladala hilo na kutoa lugha ya vitisho hivyo hakuna daladala au gari lolote lililosimama katika eneo hilo kutokana na eneo hilo kuthibitiwa na vibaka hao.

Baada ya kuhakikisha wametupora kila kitu walitokomea kusikojulikana wakiwa na funguo za gari, na kutokana na juhudi za dereva wa basi lile na kondakta wake walifanikiwa kuliwasha basi letu na tukaenda moja kwa moja hadi kituo cha polisi pale Tandale.

Tulipofika na kutoa ripoti, askari wa zamu waliokuwepo pale kituoni walimshambulia dereva wa basi letu na kondakta wake kuwa ni wazembe kwa kuwa lile eneo linajulikana kuwa ni hatari kwa vibaka ambao hupora hata mchana kweupe inakuwaje yeye asimame kituoni hapo alifajiri yote hiyo? Walidai kuwa madereva wote wa mabasi yanayopita njia hiyo wanalifahamu eneo hilo ambalo wamelipachika jina la mahakama ya simu kutokamna uporaji wa simu uliokithiri katika eneo hilo la Kwa Mtogole.
Karibu abiria wote tuliokuwa pale kituoni ambao tumeporwa tulishikwa na mshangao, kumbe eneo linajulikana kuwa lina vibaka, sasa kwa nini hawathibitiwi na kituo cha polisi hakiko mbali na eneo hilo?

Tuliandikisha maelezo yetu kisha kila mtu akashika njia yake, mimi ilibidi nirudi nyumbani ili kutengeneza uji mwingine wa mgonjwa kwani uji niliokuwa niupeleke kwa mgonjwa umechukuliwa na vibaka.



Habari na msimulizi wetu........................
 
Kwani hao polisi wana tofauti gani na muungwana? Anasema ana list ya Dons wa drugs yet mzigo unaendelea kudondoshwa hapa nchini, list ya corruption sharks yet libeneke linaendelezwa. So polisi pia wanajua mchezo wa eneo hilo, lakini ndo wanajitia kuchukulia poa tu
 
HIYO TAHARIFA MLIYOPELEKA POLICE NI HABARI NJEMA SANA KWA POLICE KWANI WANAUHAKIKA ZOEZI LA MAANA LIMEFANYIKA NA ANAUHAKIKA WA KIASI FULANI CHA MGAO

Poleni sana ndo bongo hiyo
 

Awali ya yote, pole sana ndugu yetu vukani kwa yaliyokukuta wakati bado una mzigo mzito wa kuuguza.

Swali langu kubwa ni jee tunao polisi nchi hii worth to be called that name??? Mnaripoti halafu ninyi ndo mnashambuliwa na kuambiwa kuwa kuwa eneo hilo linajulikana kuwa ni hatari kwa vibaka. Kama wanajua oilisi wamechukua hatua gani. Polisi anasema hivi akiwa amevaa kofia yenye kauli mbiu usalama wa raia, ni usalama gani wa kujua kuwa pale kuna vibaka halafu hawachukui hatua zozote.

Inatia kinyaa.

Mwema wake up, Malalamiko mengi kwako kulikoni musoma, watu kufa ovyo vituoni, majambazi kuuwawa badala ya kukamatwa na watu kubambikiwa kesi na kuwekwa rumande bila makosa.
 
hicho kieneo ni km hakuna serikali kabisa nilishuhudia live jpili moja saa kumi na mbili asubuhi pale mbele ya tanesco jamaa watatu waliopandia sweet corner wakaomba msaada pale, dereva akapunguza mwendo kidogo wa kwanza aka drop wa pili akavuta pochi kwa nguvu ya dada mmoja aliyekuwa amekaa karibu na mlango akadrop watu wanapiga kelele mwizi, dereva akaongeza mwendo imagine toka pale aliponunua mwarabu mbele ya tanesco mpaka kwa mtogole anasimama eti anauliza kuna mtu kaibiwa? dah nilishangaa lkn kuna jamaa akaniambia wanajuana hao. hiyo ndo tandale uzuri. nikiwa fisadi one day ntawahamisha wote pale halafu najenga apartments za ukweli
 
HIYO TAHARIFA MLIYOPELEKA POLICE NI HABARI NJEMA SANA KWA POLICE KWANI WANAUHAKIKA ZOEZI LA MAANA LIMEFANYIKA NA ANAUHAKIKA WA KIASI FULANI CHA MGAO

Poleni sana ndo bongo hiyo
ni kweli ndugu yangu nakumbuka mwaka 2000 hapo magomeni kona ya makanya nshawai kupigwa roba ya mbao asubuhi saa 11 sitasahau,nilikabwa,kisha nikapigwa na ubao wa kichwa na mangumi ya kuua ya usoni mpaka nikazimika,jamaa wakachukua mali za karibia milioni nilizokuwa nazo,namimi uvivu tu wa kuchukua taxi mida hiyo uliniponza,jamaa walikomba viatu,simu,wakavua cheni zangu na saa mpaka viatu,kisha wakanibwaga mtaroni,matax dreva wanaangalia tu wala hawana habari,nimezinduka baada ya nusu saa watu wananishangaa walidhani nimekufa
nimeenda kutaarifu polisi wakaanza kusema ooh,lile eneo hatari tumetoka hapo mda si mrefu na jamaa wamekukaba ngoja tuwafatilie na majina wakawataja,kwa ujumla polisi bongo ni uozo na wanafanya dili na vibaka
 
 
Pole sana,

Kuna umuhimu wa kuingia bongo na kimguu cha kuku, lowlives kama hawa wakikusogelea unateketeza wote, una aim to kill.

Najua kuna watu watasingizia social condition and all, lakini bongo kuna kujidekeza kwingi tu. Nchi mipori kibao watu wazima wanaiba hata hawana aibu.
 


Kiranga miguu ya kuku hata huku ipo. tatizo ni urasimu katika kumilikishwa.
 
Tatizo liko wapi kama polisi wanajua eneo lile ni hatarishi kwa nini hawachukui hatua muhimu??? Kweli jeshi la polisi ni zaidi ya tulijuavyo..................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…