Dar es salaam na 'kaimu mkuu wa mkoa'

kani

New Member
Mar 3, 2011
2
0
Kwa muda mrefu sasa,jiji la dar es salaam limekosa mkuu wa mkoa! Toka baraza la mawaziri litangazwe,ambapo Ndg. William Lukuvi aliyekuwa anashika nafasi hiyo alipoteuliwa kuwa waziri-ofisi ya raisi Bunge,jiji hili liko chini ya mtu anayekaimu tu! Maswali yafuatayo yanajitokeza
Hivi kuteua mtu tu nayo ni kazi? Au hatuna 'shemeji aliyebaki' au bado wanasoma?
Je kama tunaweza kukubali jiji kubwa na lenye umuhimu kitaifa na kimataifa likaimiwe, je wakuu wa mikoa wana umuhimu kweli?
Mimi nashindwa kuelewa wana JF nisaidieni!
 
mkwere amesahau kama anatakiwa ateue wakuu wa mikoa anasubiri wasaidizi wake wamkumbushe, very useless him & his co.
 
Na Manyara pia haina RC. Said Meck Sadiq ameweza lakini. Hana ngonjera nyingi kama waliomtangulia. Hivi yule mzee ni zeruzeru au rangi yake tu?
 
tetesi ni kwamba mzee tibaigana ndio anatayarishwa kua mkuu wa mkoa huu
 
It shows that we can move on without RCs....they are useless with the DCs....The RAS is doing the donkey work an the RCs keep on yakking
 
Hapa ndiyo inadhihirisha kuwa kumbe ma DC na ma RC hawana umuhimu wowote zaidi ya kuwa mzigo kwa walipa kodi, Chadema wameona mabali kwa kusema kuwa wao wakiingia madarakani wanafuta vyeo hivi. Au tuseme ndiyo JK anaanza kutekeleza sera murua za Chadema, na kwa kutoteua RC wa Dar anafanyia majario, well done JK, usione haya kutekeleza sera zetu kwa manufaa ya Taifa letu.
 
Hivi vyeo vya mkuu wa mko,mkuu wa wilaya,naibu waziri havina maana yoyote vinatakiwa vifutwe kabisa
 
Jamaa anasubiri abadili wakuu wa mikoa na kuunganisha na ma RC wa mikoa mipya minne, na atabadili pia wakuu wa wilaya na kuchagua wengine kwa kujumuisha wilaya mpya 17.
Hivi mnadhani UVCCM kutoa matamko na mbwembwe kibao waonekane wanakipigania chama unadhani juhudi hizo ni za bure? WILAYA mpya 17 zinawatoa ROHO wanataka waonekane ili wakumbukwe katika UTEUZI. KAZI zenyewe za URC na UDC ni ukada wa chama tu hamna kazi yeyote yenye tija kwa Taifa kupitia nafasi hizo ndio maana MADOGO hao wanapigania nafasi hizo za MDEBWEDO
 
Kwa muda mrefu sasa,jiji la dar es salaam limekosa mkuu wa mkoa! Toka baraza la mawaziri litangazwe,ambapo Ndg. William Lukuvi aliyekuwa anashika nafasi hiyo alipoteuliwa kuwa waziri-ofisi ya raisi Bunge,jiji hili liko chini ya mtu anayekaimu tu! Maswali yafuatayo yanajitokeza
Hivi kuteua mtu tu nayo ni kazi? Au hatuna 'shemeji aliyebaki' au bado wanasoma?
Je kama tunaweza kukubali jiji kubwa na lenye umuhimu kitaifa na kimataifa likaimiwe, je wakuu wa mikoa wana umuhimu kweli?
Mimi nashindwa kuelewa wana JF nisaidieni!

Mie issue ni huko LINDI ambako KAIMU RC wetu ndio kituo chake cha kazi ina maana nao WANAKAIMIWA TUU kama sisi.....???
 
Mie issue ni huko LINDI ambako KAIMU RC wetu ndio kituo chake cha kazi ina maana nao WANAKAIMIWA TUU kama sisi.....???

Kwa nini maDC wa mkoa husika wasikaimu nafasi hizi? Jordan Rugimbana wa Kinondoni angefaa sana kuwa Kaimu RC wa Dar. Gama wa Ilala kama Komba wa TOT!
 
tetesi ni kwamba mzee tibaigana ndio anatayarishwa kua mkuu wa mkoa huu

mara ya mwisho nlipata taarifa kuwa mzee Tibaigana kakataa uteuzi huo,kuna afsa uhamiaji mmoja ambaye alikuwa anajiandaa kuwa kampeni meneja wake ila Mama Tibaij uka akazidi kura za maoni,alisema mzee Tiba hataki uteuzi wowote kwanza apumzike,labda kama wameshakubaliana. Ila kwa upande wa pili ndo huone kuwa kuwepo maRC ni kutengenezeana Ulaji. Kama nusu mwaka mkoa hauna Rc na uko salama,si bora cheo kifutwe?
 
Yupo mtu anaKAIMU jamani. Ana nguvu zote kiutendaji. Sio kwamba mkoa hauna RC.
 
hivi mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya kazi zao ni zipi? si ajabu hata jk haoni umuhimu wao, maana hata kamati za kudumu za bunge zinawachachamalia wakurugenzi wa wilaya na si wakuu wa wilaya au kada yo yote ya mkoa.
 
Labda cha kudodosa hapa ni gharama za kumweka hoteli Kaimu RC kwa muda wote huu wakati shule zetu hazina madawati!
 
Kwa nini maDC wa mkoa husika wasikaimu nafasi hizi? Jordan Rugimbana wa Kinondoni angefaa sana kuwa Kaimu RC wa Dar. Gama wa Ilala kama Komba wa TOT!

sijakuelewa kijana, hebu fafanuwa hapo kwenye RED, nikiamka nikute jibu.
 
hivi mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya kazi zao ni zipi? si ajabu hata jk haoni umuhimu wao, maana hata kamati za kudumu za bunge zinawachachamalia wakurugenzi wa wilaya na si wakuu wa wilaya au kada yo yote ya mkoa.

Ni mtiririko tu wa madaraka na majukumu ya Rais kuyasogeza karibu na WANANCHI. RC anatajwa kwenye katiba ya JMT.
 
ni kweli ukiangalia kwa makini na kuainisha majukumu yao watu hawa (dc,rc,naibu waziri) hawana haja ya kuwepo.ktk mabadiliko ya katiba mpya posts hizo iko lazima kuziondoa. mathalan, mtendaji mkuu wa wizara anatajwa kuwa katibu mkuu wa wizara halikadhalika kwa ded alivo ktk wilaya. so clearly unaweza kuona kusivo na haja ya naibu waziri,rc,dc as far as ukubwa wa serikali na gharama za kuendesha is concerned
 
Back
Top Bottom