Dar es Salaam Mpya: NSSF kuanzisha miradi mikubwa jijini; Mwisho wa malori kuingia jijini wawadia

Mabadiliko muhimu,tusonge mbele mtu anpokuja na idea nzuri ya kuboresha jambo tumpe sapoti.nchi nyingine wanasonga mbele so let us!
 
Kwanini NCCF WASINGEWAJENGEA WANACHAMA wao kwanza nyumba za bei nafuu kuliko kuwaacha wakihangaika huku pesa zao ya makato yakitumika kunufaisha wengine. Ni vizuri kama wangejenga nyumba kwa wanachama halafu wakawauzia au kuwapangishia kwa gharama nafuu. Mwanachama angepata unafuu na kunufaika na chama kwa upande wangu nilidhani watu muhimu kwanza ni wenye chama halafu unaelekeza mikakati mingine kwa kwingine. Utaachaje nyumba yako ikiungua na kukikimbilia kuuzima wa jirani.
 
Imagine huyu ni Mkurugenzi mkuu wa NSSF,wazo hili lilitakiwa kutolewa na kusimamiwa na PM ama BOss wake ila hao wote wamekaa kimya kama vile hawaoni nchi hii ina vituko sana..
 
Dar! Dar! Dar! Dar! Why not Kigoma?

Kigoma na Mwanza ipo kwenye mipango ya miaka mitano (2010 to 2015) ya JK. Kigoma ataijenga kama Dubai na Mwanza kama California.

Anyway, kama hii kitu ni kweli basi NSSF wapewe serikali na serikali wakaongoze NSSF...............!!!! $0 % ya badget inategemea Umatonya halafu hawa jamaa wanakuja na ndoto zao za kufikirika?? mpaka inaudhi.................KUDADADADADEKI!!!
 

jK alikuwa kashikwa pabaya na Dr. Slaa akaanza kuropoka oovyo
 
Mwakani lazima Nikombe pesa yangu yote, make kwa hizo project haziwezi fanikiwa bila kwanza kuondoa fao la kujitoa
 
Nilimsikia Lowasa Bunge lililoisha akipendekeza hata balozi zetu zijengwe kwa pesa ya NSSF. Hawa jamaa ni balaa na huyu DAU ni dau kweli.
 
mkuu unaweza ukawa upo sahihi, lakini hebu nitajie tu mkurugenzi mmoja katika shirika la nssf aliyemtangulia Dr. Ramadhani Dau aliyewahi kufikia mafanikio haya? na shauri ushabiki na udini tuweke pembeni.
 
Hivi Mkurugenzi wa NSSF huteuliwa na rais?

Je, rais ni mwanachama wa NSSF pia?.?

Kama sio mwanachama kwa nini wakurugenzi wanajipendekeza kwake na sio kwa wanachama??

Wewe huna akili kabisa, Hiyo miundombinu na uboereshaji wa makazi ni kujipendekeza kwa Rais? Ulitaka nae awe na kashfa za kuficha pesa nje ili uone hajipendekezi? Kichwa chako kimeumbwa kuhifadhi Mapunye kwenye bongo yako!
 
mkuu ni nani hasa mwanachama wa nssf? mimi nilikuwa mwanachama, nikatoka, nikarudi na sasa natarajia kutoka. kwa kifupi kila mtu either ni mwanachama wa nssf either mstaafu, mtarajiwa au active. think wide, hili ni jukwaa la maGT
 
Mwakani lazima Nikombe pesa yangu yote, make kwa hizo project haziwezi fanikiwa bila kwanza kuondoa fao la kujitoa
sishangai wewe ukawa graduate wa UDOM au umeishi mabibo hostel, chuo cha hombolo et al. ambazo zimejengwa na NSSF. utafikiri ana kichwa kumbe ni kifuu cha nazi kipo juu ya shingo.
 
ujinga unakusumbua. NSSF inawekeza. sasa kuhamisha makao/ofisi kwenda dodoma kutarudisha vipi hizo hela. ukimwona utafikiri anakichwa kumbe ni kifuu cha nazi.
 
unaongea as if wewe peke yako ndo unachangia pale NSSF. na si shangai wewe ukawa graduate wa udom. kwa kweli mimi kwa haya wayafanyao nakubaliana kabisa nao, japokuwa najua watendaji wa nssf hasa hawa wa chini ni wasumbufu sana. tanzania tuko nyuma sana kimaendeleo, kwa hiyo hatuna budi kutumia kila opportunity tuipatayo. otherwise we are finished.
 
..serikali imeamua kujenga bandari BAGAMOYO.

..mradi wa bandari ya nchi kavu Kisarawe ni wa nini?
 
Watu wanaoishi MANZESE na VINGUNGUTI wataenda WAPI? Isije Ikatokea kama SLAMs za NAIROBI kwa Wananchi kufukuzwa kwenye VIWANJA halali...

Kwanini kila kitu KISARAWE??? BANDARI MPYA ITAKUWA HUKO as WELL
Kwanini wasingesogea CHINI KULIA kwa BANDARI yetu IPO LINDI inahitaji MAENDELEO Oh LINDI ni kwa MAMA; Kisarawe kwa BABA... Mmmmmmmmmm
 
ujinga unakusumbua. NSSF inawekeza. sasa kuhamisha makao/ofisi kwenda dodoma kutarudisha vipi hizo hela. ukimwona utafikiri anakichwa kumbe ni kifuu cha nazi.
Naona uliamka vibaya leo mkuu....msongamano Dar ni tatizo...kiuchumi ,kijamii. Kikwazo cha serikali kuhamia Dodoma tunaambiwa ni gharama. NSSF pia ina wajibu wa kutoa huduma hasa pale kwenye tatizo. Nilichotaka kusema kama imeweza kuikopesha serikali katika miradi kadhaa...haiwezekani pia kufanya hivyo kupunguza hili tatizo???.........
 
Naipongeza NSSF kwa mpango mzuri wa kuboresha jiji, lakini huu mpango wa kuboresha uswahilini unatia mashaka kwa sababu fidia watakazolipa zitakua ndogo sidhani kwa nyumba ya kawaida itafika hata 50M wakati NSSF ikishajenga itakwambia nyumba ya gharama nafuu wanauza 100M kama wanavyotufanyia sasa NHC wanasema wamejenga appartment za gharama nafuu ukiuliza bei unaambiwa 100M Je mtanzania gani ataweza nunua hizo nyumba km sio wafanyabiashara halafu watupangishe kwa USD.

Mtanzania aliyefidiwa 50M leo baada ya miaka 2 mradi ukikamilika atakua amebakiza pesa kidogo hataweza kunua hizo nyumba hata akiambiwa alipie nusu bei.

Watumishi wa umma wengi hatutaweza hata tukikopa kwa sababu zaidi ya 80% ya mafao yataishia kulipa deni la nyumba tutastaafu tukiwa na pesa kiduchu!
 
Gazeti la mwananchi leo: NYUMBA ZA BEI NAFUU NSSF NI SH200 MILIONI. Zimejengwa ili kuwauzia wanachama wake kwa bei nafuu eneo la Kijichi Dar. Je kuna huwino wa haya yaliyosemwa ZNZ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…