Dar es salaam kuna tatizo bado! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar es salaam kuna tatizo bado!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paul Kijoka, Apr 2, 2012.

 1. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kinachotukwamisha kisiasa Dar kuna wajinga wengi, misukule mingi, mbumbu wengi,
  mateja wengi na zaidi walala hoi wengi. pia kuna watu wengi wanaojifanya wako bize kuliko eneo lolote TZ.
   
 2. A

  Afghan Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo siyo hilo, Dar wengi ni waajiriwa na kama si mwajiriwa basi yuko attached na program fulani ya fisadi mmojawapo ndani ya serikali. Ukizungumzia mikoa inayoonekana kifua mbele katika mapambano wengi wana deal zao binafsi na wanapambana kivyao.
   
 3. e

  ebrah JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo Simo hill, tatizo dar haina mwenyewe! 80%ni wahamiaji,na kwa sababu hiyohakuna umoja, Makabila yenye nguvu majority ni watu wa kabila moja na luggage moja so ni rahisi kuelrwana na wanauchungu na kwako, huku mtu anajali Tumbo na familiar yake! ana.
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ni MISUKULE, hii nimeipenda zaidi
   
 5. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,705
  Likes Received: 2,388
  Trophy Points: 280
  Mhh ndugu na wewe hizi ni typo error au ndio kabila na lugha tusiyoijua na huko utokako tusikokujua maana kwako wewe umoja na mashirikiano lazima muwe dini, moja kabila moja ,ukoo mmoja, familia moja, baba mmoja,tumbo moja, jinsia moja aina moja ya kiumbe na ujinga mwingine unofanana na huo.maana sijui hiyo dhana ya uhamiaji na mji kama na Dar wenye umri wa miaka zaidi ya 200 unaifahamu!
   
 6. M

  Mbinga Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nadhani wadau hapo mnakosea kufikiria hivyo. Kumbuka wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 majimbo yote yalikuwa yametwaliwa na upinzani kama siyo ujanja wa CCM kulazimisha uchakachuzi! Hata hivyo ukiangalia Jimbo la Kawe, Ubungo, Temeke na kule Segerea utagundua wakazi wa Dar wako makini kuleta mabadiriko
   
 7. m

  mchungusana Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 15
  Asa asa temeke hakuna lolote yani ndo ya mwisho kimaendeleo lkn wanang'ang'ana na Mtemvu(ccm), wanaboa sana
   
 8. k

  kiomboi JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  wanahitaji maombi!!
   
 9. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wadau, naomba nitoe angalizo. Si kwamba watu wa Dar ni wapuuzi au wajinga La Hasha, hapa chadema tuna majimbo mawili. Pili tufahamu ili mtu aweze kuchagua upinzani lazima apewe elimu ya uraia. Nikirejea mikoani kuna Operesheni nzito zilianzia Kanda ya Ziwa (operesheni Sangara mwiaka ya 2008 hivi) na hapo tukaona matokeo 2010, pia Operesheni hiyo ikaendelea Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini matokeo tunayaona Songea sasa ni Ngome yetu na Iringa (Mby siisemi ni ngome ya upinzani siku zote), Tukaenda Igunga mkaona matokeo, juzi kamanda wetu Zitto kaenda Tanga kaendesha awareness campaign nzuri.

  Naomba muelewe hii ni vita hivyo tunapigana battle baada ya battle ndio unashinda war.
  Ushauri - Operesheni Sangara ilenge maeneo yafuatayo ambayo bado ni ngome ya CCM, Morogoro, Dodoma, Dar, Pwani kisha tuvamie Kusini ili tuwe tumezunguka nchi nzima.

  Swali - je wewe kama mwana chadema umesaidiaje kuelimisha wananchi juu ya ukombozi wa nchi yetu, kumbukeni tusiishie kushabikia hapa JF tuende mbali zaidi hususani huko Temeke ili tuwaandae wanachi na 2015. nwaoma kuwasilisha
   
 10. m

  majogajo JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  na masharobaro wengi....isitoshe wao ndo wanaopigwa na maisha.
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Huijui Temeke kisiasa, kwahiyo nyamaza!
   
 12. w

  wakwetu 2 Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kweli coz waswahili wengi ila si kote haswa kwenye watu weamba wenye maisha magumu ndio ngome za magamba- uswaz ndio wanat fofaut na ushuani kama segerea, tabata, mbez zote,ubungo,kimara, kinyerez nk tofauti na manzese, kigogo kijibweni,nk
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,997
  Likes Received: 23,899
  Trophy Points: 280
  Dawa kwa hapa Dar ni kuchapana makonde tu. Kuna mijitu bila kubwengwa mikwenzi haibadiliki. (source: mizee michovu ya Dar kwenye matukio ya Rais kuongea umbea na wazee wa Dar)
   
 14. p

  petrol JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Kama hujui, ubwabwa unadumaza akili.
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280

  Afadhali umeongea ukweli...na ni ukweli huu ambao mara kwa mara nimekuwa nikiuzungumza hapa jukwaani ingawaje wapo wasiotaka kuelewa au hawataki kukubali ukweli huu! HUu ni udhaifu mkubwa sana kwa CHADEMA na mashabiki wake wengi ambao kimsingi wamekurupukia tu siasa wamekuwa hawauoni ukweli uliouzungumza! Mashabiki hawa ambao mie nawaita mamluki wa siasa wamekuwa tu wakiishia kuwakashifu wananchi wasiochagua upinzani kwa kuwaita hawana elimu, wavaa misuli na upuuzi mwingine kama huo! Wanasahau kwamba wananchi nao wapo smart....hawawezi kumchagua mtu ambae haoneshi interest yoyote kwao! Chukulia uchaguzi 2010, mgombea wa CHADEMA TMK (ubunge) alipata kura nyingi sana ambazo mie nilishangaa kwamba alizipata pata vipi coz' CHADEMA hawakufanya hamasa yoyote ya maana TMK mbali na ule mkutano mkuu pale Mwembe Yanga ambao mgombea yule aliishia tu kuporomosha matusi kwa JK! Maeneo mengi ya TMK hayakuwapo hata mabango ya kumnadi Slaa lakini bado mtu asiyeelewa anaishia kuwalaumu wananchi kwa kuzani kwamba wao ni watu wa kukurupukia tu na kushabikia wasichokijua!! Nenda maeneo kadhaa ya pwani; huko huwezi kukuta hata ofisi ya CHADEMA, lakini bado mtu anazani wananchi hao watachagua tu CHADEMA....huu ni upofu wa ufahamu! Kwa hapa Dar, hakuna wilaya yoyote mbali na Temeke ambayo majimbo yake yote yameshawahi kukaliwa na wapinzani....!! Kwenye uchaguzi mdogo after 1995 general election, TMK ilichukuliwa na NCCR Mageuzi chini ya Mrema...na kwa vipindi viwili tofauti; Kigamboni ambayo nayo pia ni TMK iliwahi kuchukuliwa na CUF chini ya Tambwe Hiza na Frank Magoba! Wote hao, hakuna cha maana ambacho walikifanya na badala yake waka-prove kwamba ni mamluki tu!!! Watu wanaiona TMK wakati Ilala na Kinondoni hawajawahi hata mara moja kuchagua upinzani...!!

   
Loading...