Dar es salaam-Kinshasa Railway lazima ijengwe

mkuu hiyo reli kutoka dar hadi kinshasa itapita wapi? malawi au ruanda?? wote hao maadui zetu

wewe utakuwa unawaza kwa kutumia Ma------ kwani Malawi haipakani na DRC, hivyo point yako inakuwa batili hata kabla ya kuifikiria, pili Joyce hana akili mbovu, ndio ana matamanio lakini anajua anachoweza na asichoweza ndio maana haonge ovyo ovyo, au kufanya vituko ku discredit majirani zake, na pia ndio maana Chisano anaendelea na usuluhishi.
Tatu tunaweza kupitia Zambia ambapo reli ipo kwa sasa au kutumia Kasanga Port. Mpaka hapo au bado akili ipo......?
 

Naona unatimua vumbi tu Mkuu!Sijui ulikuwa bado una hasira ya kugombezwa na Boss wako kazini wakati unaandika hii post?Ungelala kwanza akili itulie kabla ya kuchangia!!!LOL!!!
 
Naona unatimua vumbi tu Mkuu!Sijui ulikuwa bado una hasira ya kugombezwa na Boss wako kazini wakati unaandika hii post?Ungelala kwanza akili itulie kabla ya kuchangia!!!LOL!!!
naona una mtetea mkeo/mumewo kwa kuandika utumbo usio husiana na hali halisi ya bongo na mikakati ya Tz kupambana na watu wenye akili ya vita vita na wizi
 
Ni ukweli mtupu lakini kinachotakiwa kwanza ni kuwaondoa manyang'au madarakani kwanza . Tumeshindwa kuitumia reli ya Tazara kwa uroho tu wa rushwa
 
mkuu hiyo reli kutoka dar hadi kinshasa itapita wapi? malawi au ruanda?? wote hao maadui zetu

Congo ni kubwa sana kulinganisha na nchi zote za EAC. Hata hivyo tusisahau kuwa Congo tulishakuwa nao zamani kibiashara. Kujitoa kwa Rwanda na Uganda ni kupoteza Biashara

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Congo ni kubwa sana kulinganisha na nchi zote za EAC. Hata hivyo tusisahau kuwa Congo tulishakuwa nao zamani kibiashara. Kujitoa kwa Rwanda na Uganda ni kupoteza Biashara

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Asante kwa kuliona hilo mkuu, lakini tusijitoe huku north ila tujiongezee wigo wa kibiashara.
 
mkuu hiyo reli kutoka dar hadi kinshasa itapita wapi? malawi au ruanda?? wote hao maadui zetu
Asante kwa ramani hii, lakini wadau wanasahau kuwa reli hii ya Dar-Kinshasa kwa upande wa Tanzania tayari ipo(Dar-Kigoma).
Vile vile wengine wanasahau kuwa Ziwa Tanganika si kikwazo kwani hata hapo zanani reli ya Dar-Mwanza-Entenbe ilikuwa inafanya kazi vizuri tu kwa kuwa na railway ferries zinazo ishia Port Bell Uganda.

Lazima miradi hii mikubwa ibuniwe na tusingoje wengine wachukue initiative na waka take advantage ya kulala kwetu.
 
Unafikiri kuwa nchi ya Congo haina Bandari?
Tazama vizuri ramani na utaona kuwa toka east Congo ni mbali zaidi hadi Kinshasa kuliko kwenda Dar.

Na ninavyozungumza sasa, ukienda Tunduma zaidi ya 40% ya mixingo inayotoka nje inaenda Kongo.
Tuchangamkie fursa.
 
Watekelezaji hii miradi ni wakina nani au hayahaya maccm yanayouza kila kitu, tuache juhidanganya na ndoto za alinacha na vimbelembele vyetu
 

Naungana na wewe Mkuu katika hili South Africa wameshaanza kuwekeza na Zuma alikuwa huko Majuzi na wamekubaliana kujenga Bwawa la Umeme na ushirikiano wa Kibiashara.Tatizo letu ni kwamba bando tuna syndicate ya kimatonyamatonya na hatujielekezi kuwekeza kwa kutumia fursa tulizonazo zaidi yakuzunguka zunguka ulaya. Hapa siyo kuimarisha Reli tu iwe nipamoja na kuwawezesha wafanya Biashara wadogo na Wakati kujipenyeza huko na kufanya shughuli za kibiashara .Pia kuboresha upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji kwa kuweka Mikopo ya Riba Nafuu.
 
mkuu hiyo reli kutoka dar hadi kinshasa itapita wapi? malawi au ruanda?? wote hao maadui zetu


Sio lazima reli kufika mpaka Kongo kabisa. Unaweza ukaishia lake Tanganyika on our side na kwa upande wao. Jenga bandari on our side and on their side.
 

Thats the spirit mkuu
Lazima siasa zetu zilenge kwenye kufaidika kiuchumi.
Siyo siri katika miaka ya huko mbele Kongo itakuwa a giant economical power house, na sisi tujiweke kufaidika.
 
Mawazo mazuri sana, ila sisi bado si watu/nchi ya kibiashara. Tuendelee kufikiri vizuri huku tukiamsha Ari na Mazingira ya kibiashara. Serikali ifanye bishara yenyewe, kupitia mashirika yake, na makampuni ya kitanzania haya haya madogo madogo yawezeshwe, kuweka mazingira bora kabisa kwa watz wengi zaidi kufanya biashara. Ili Hizi fulsa zipate kutumika bara bara. Haya yote yanawezekana ni uthubutu tuu ndio tumekosa.
 
Yote yaliyozungumzwa ni mema na mazuri,ispokuwa kabla ya yote tanzania haina budi kuisaidia drc,1> ktk kuimarisha jeshi lake pamoja na kurecruit vijana wenye origin ya kongo wasio na damu ya kitutsi,2>kuimarisha
mfumo bora zaidi kiusalama wa ndani ya drc 3>kunutralise vikosi vyote vidogo vidogo vya waasi pamoja na kunyanganya silaha zote 4>extend democracy and so so
 

Mkuu viya isivyoisha Kongo ni sababu ya umasikini.
Wakianza kujenga reli hii hata hao wapiganaji wataajiriwa kwa kipato kizuri tu bila kujali ni kabila gani.
Lakini ni kweli usalama lazima uhakikishwe, na naona hilo linaonekana wazi kwa matukio ya Goma na jinsi M23 walivyo shughulikiwa.
Kongo ikiamua inaweza.
 
Maamuzi yoyote ya jazba na kukomoana yatatucost sana kwa kuwa viongozi waliopo madarakani ndio wanaobadili upepo wa mahusiano baina ya nchi na nchi! Iam sure wakiondoka tu madarakani utaona upepo utakavyobadilika. I think we need to be careful kabla ya kuanza kuingiza mipesa yetu kisha yakaishia njiani kama tulivyoanza kuwekeza kwenye miuondombini na Rwanda. Tuache siasa za visasi............Ya ngoswe mwachie ngoswe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…