Dar es salaam: Kikwete kufungua barabara ya Mwenge - Tegeta

Dar es salaam: Kikwete kufungua barabara ya Mwenge - Tegeta

Ila ukilinganisha na lile foleni la barabara moja...ni afadhali kidogo kwakweli japo magari kila siku yanaongezeka
 
Katibu mkuu anaendelea kwa hotuba yake kwa kuwashukuru Japan kwa misaada yao kwa Tanzania
 
amesharudi kutoka USA chadema bado maandamano yapo pale pale hizo barabara hazina faida kwetu
 
Katibu mkuu anamkaribsisha mhe.rais anapanda jukwaani sasa msondo wanatumbwiza mhe rais naongea na wananchi mhe.rais anamchukuru waziri wa ujenzi kwa kumialika kwenye shughuli hii
 
Mhe.rais anaipongeza serikali ya Japan kwa msaada yako kwa watanzania
 
Mbunge wa kawe Halima mdee jukwaa mkuu akijumuika na viongozi wengine wa serikali
 
Kikwete anahoji kwanini ujenzi wa mabasi ya kaskazini kinachotakiwa kujengwa tegeta bado kuanza
 
Barabara acha zijengwe ila inabidi serikali iunde chombo cha kusimamia haki na maslahi ya vibarua na wafanyakazi wazawa wa kampuni hizi za ujenzi wa barabara, kwani wamekuwa wakiburuzwa na hakuna wa kuwatetea wamekuwa kama wakiwa vile. Waziri wa kazi na ajira, huku katika sector hii hata hakuoni na sijui kama anajua kuna madudu yanafanyika. Mh Magufuri na hata Mh. Rais wao kazi yao ni kuizindua tu tena kwa mbwembwe lakini hawajui kuwa miongoni mwa waliojenga wapo taabani kwa maumivu ya malipo madogo. Na ndiyo maana wengine wasiokuwa na uvumilivu wanaamua kuiba mali za kampuni kama mafuta, cement, nondo, vifusi, zege na n.k. Ili kukidhi mahitaji yao kwani mishahara wanayopata ni midogo sana. Baadae baada ya kugundua kuwa wanaibiwa huenda kulalamika kwa viongozi wa serikali, Na hao viongozi wakija wanapiga kelele bila kujua kwanini watu wanawaibia. Naomba liangaliwe hili.
 
Kikwete asema foleni nyingi zinawafanya watu wasitimize miadi yak kwa wakati
 
Hiyo project nilikuwa mfanyakazi lakn niliacha kwa uhuni waliokuwa wanatufanyia,nilikuwa dereva wa project manager nikashindwa.
 
Kikwete aahidi kujenga train kwa ajili ya usafiri wa dar na flyover kwenye makutano mbali mbali ya barabara
 
Korea kusini kujjenga daraja kutoka aghakhan hospital hadi coco beach kupitia baharini kikwete anena
 
Watu hawajui matatizo wanayokutana nayo Wabongo katika kampuni hizi za ujenzi, hapo wamejaa wanashangilia ufunguzi, barabara imependeza lakini we acha tu, pole GODFREY KIMI. Ingekuwa kuna utaratibu wa kuwasikiliza wafanyakazi yao machache hata katika hafla ya ufunguzi kama hii ya leo, wangeumbuka watu kwa kweli maana wangefichua uozo na uovu na madudu yote.
 
Back
Top Bottom