Dar es Salaam: Jiji lililotapakaa pombe kila sehemu!

Dar es Salaam: Jiji lililotapakaa pombe kila sehemu!

ngoja nijipitie zangu tyu.hayanihusu haya!!!
 
Jiji la Dar ni jiji lenye umaarufu lenye uchangamfu wa biashara na huduma mbali mbali! hii imechangiwa na uwepo wa shughul za serekali pamoja bandari.

Cha kushangaza jiji hili limekumbwa na uuzaji holela wa hasa za kwenye karatasi (viroba) hali inayopelekea unywaji wa hovyo wa pombe hizo! Tofauti na nchi nyngne pombe hzi hupatikana karibu kila sehemu na haijalishi ni bar au lah!!

Hupatikana kwa wauza karanga barabarani, maduka ya vyakula, grocery, vituo vya daladala! Cha kushangaza hadi mama ntilie ni wauzaji!

Unywaji Wake nao ni wa tofauti wapo wanaonywea oficin(wanazuga wanaenda chooni), kazini(dereva wa bodaboda na magari), wakitembea njian (hubeba mifukoni)! Umri hauzingatiwi hadi wanafunzi wa shule za msingi ni walevi wa pombe hizi.

HATARI: Nyingi ya pombe hizi hazitengenezwi viwandan bali hufojiwa kienyeji mtaani, hali inayopelekea kutokuwa salama kiafya.

John Pombekali Magufuli #HapaZikaTu
 
Mimi naona limejaa au kutapakaa uchafu wa mifuko ya plastiki
 
Wenye matatizo yote ya kiafya ni wanywaji?!


Sasa kama wenye matatizo yote ya kiafya hayakusababishwa na unywaji ndio inakupa wewe jeuri ya kunywa vitu vyenye hatari na Afya yako? Hasa hivyo Viroba vinavyotengenezewa mitaani? Kaa chini ufikirie na Ujihurumie mkuu..Ni ushauri tu.
 
Kwani we kinakuuma nini wenzako kunywa maji??

Kinamuuma anaona nguvu kazi inapotea kwa kunywa pombe zinazotengenezwa mitaani bila vipimo wala utaalamu, kumbe wewe unaweza kumuona mwenzio anaenda kudumbukia shimoni na ukamuacha tu eti kisa hakikuumi kitu? Au haikuhusu?

Binadamu sote ni ndugu na ni vizuri kushauriana mazuri na mabaya na hayo ndio maisha,

Don't be selfish
 
Sina jib sahihi sababu sijawahi kuishi Mbeya! Ila inaonekana ni tatizo la nchi nzima!

Hapo Usihisahau Arusha Huko Nako Ni Shida Unywaji Wa Viroba Unaitwa Kukatia,machalii Wanakatia Mbaya.Bora Mabadiliko Yaje Unywaji Wa Viroba Upungue Watu Waanze Kukatia Bia
 
Acha tunywe!kama mambo yetu yanatunyookea kwani ni nini mbaya?

Tatizo sio unywaji ila upatikanaji wake una walakini! ona had wanafunz wa primary wanatumia je kuna mustakbal gan katika masomo yao?
Afya zinadorora nguvu kazi zinapungua asubuh 2 wamelewa
 
Back
Top Bottom