Dar es Salaam ifanywe mji mkuu msaidizi, Dodoma itaanza kupokea ugeni mkubwa lini?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,260
Tangu awamu ya tano na sasa ya sita wageni wakubwa wa nchi wamekuwa wanapokelewa Dar na matukio makubwa yanafanyikia magogoni japo mjii mkuu ulishamishiwa Dodoma na serikali yote ikahamia huko.

Hii ni kusema kwamba Dodoma na miondombinu ya mji huo huenda bado haikidhi kupokea wageni wakubwa?

Kama ni hivyo kuna huja ya watunga sheria kutunga sheria ya kuifanya Dar es Salaam mji mkuu msaidizi wa nchi. Iwe kwamba mawaziri na watendaji wakuu wa serikali kuu wanaosafiri kuja Dar es Salaam kutoka Dodoma wanahesabiwa bado wako katika kituo chao chao cha kazi cha Dodoma.

Hii inamaanisha hao viongozi wasipewe posho zozote za safari wanaposafiri kati ya Dar na Dodoma ili kulipunguzia taifa mzigo wa kuhudumia miji mikubwa miwili ambayo yote bado inatumika kwa shughuli kubwa za serikali zinazohusisha viongozi wakubwa wa nchi.
 
Una haraka sana

Ngoja uwanja wakimataifa ukamilike (Msalato International Airport)

Ikulu ikamilike pia

Balozi baadhi zime anza kufungua ofisi, tusubiri balozi Zikae sawa pia

Miundombinu mbalimbali ina endelea kujengwa

Na ofisi mbalimbali zina endelea kujengwa

Kwa ufupi jiji la Dodoma lina jengwa lina jijenga na litakapo kamilika basi unayo yasema yatakuwa na majibu tayari
 
Back
Top Bottom