Dar es Salaam : Hamna Maji hata tone!!!

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,076
2,443
WanaJamii,

Mnaweza kunisaidia taarifa yoyote ambayo DAWASA waitoa kuhusu ukosekanaji wa MAJI katika Jiji la Dar es Salaam?

Ni siku ya tatu leo naona mabomba yako kimya!!!

Walitangaza wanarekebisha bomba la inch 24 pale Lugalo na itachukua masaa 12 hadi 24 hivyo tutarajie maji kutoka jumatatu ya leo nashangaa kimya. Na nashangaa ikoje mpaka wafunge Ruvu chini na Ruvu juu kwa pamoja

Ahsante kwa taarifa!

Masaa 12 mpaka 24 - mbona yamepita masaa 36 sasa?

Kama maji hakuna mheshimiwa Kyabu, Kunywa bia.

Hii ndiyo nchi yetu, na Daslam ndo mji mkuu wa kibiashara.

Kukosekana kwa maji, umeme na vitu kama hivyo ndiyo vivutio kwa wawekezaji.

Sidhani kuna maji yaliyobakia,ile jmo,nilikuta yakimwagika pale lugalo kama mafuriko!

WanaJamii,

Mnaweza kunisaidia taarifa yoyote ambayo DAWASA waitoa kuhusu ukosekanaji wa MAJI katika Jiji la Dar es Salaam?

Ni siku ya tatu leo naona mabomba yako kimya!!!

Maji yametoka sijui huko kwako! Na hapo lugalo walipokuwa wanatengeneza linamwaga maji kinoma!!! Huenda wakafunga maji tena

Kama uko karibu na msikiti kachote ya chumvi. Angalau si haba kwa kuogea....

Bora yakatike hivyohivyo ili wale jamaa mtaani kwetu wanaokata mabomba ili wayauze kinyemela wakome, ukiwauliza wanasema tatizo serikali yaani serikali ndiyo imemwelekeza akate mabomba ya maji au?

Heri yenu nyie maji hayatoki lakini mabomba yapo.
Sisi kwetu mabagala hata mabomba ya Dawasco hayajatufikia, tunatumia maji ya visima.

Heri yenu nyie maji hayatoki lakini mabomba yapo.
Sisi kwetu mabagala hata mabomba ya Dawasco hayajatufikia, tunatumia maji ya visima.

Brah? Aa yuu Rwezaura or sort of.... Sorry for any inconvinience!

"Tanzania ni moja ya nchi Duniani ambayo wananchi wake wamezoea kuishi na matatizo na kuyachukulia poa tu"

"Tanzania ni moja ya nchi Duniani ambayo wananchi wake wamezoea kuishi na matatizo na kuyachukulia poa tu"

Siyo kuyachukulia poa bali kuyafanya ya kisiasa - Nimeenda DAWASCO Makao Makuu kuulizia vipi maji yatatoka saa ngapi wakaniuliza kwani wewe CHADEMA? Nimemtukana yule Afisa mpaka nikaitiwa walinzi!

WaTz wamezoa shida sana! Hapa mtu ukianza kulalamika utaambiwa wewe wa wapi. Watu wamekomaa na ugumu wa maisha na wanaona sifa.
Shida yetu sio physical maendeleo bali maendeleo ya fikra. Tukishapiga hii hatua ya kwanza then mengine yote ni possible!!

Back
Top Bottom