Dar es Salaam: Daladala laigonga treni na kuua mtu mmoja, majeruhi 23

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,956
13,717
Mtu mmoja amefariki leo asubuhi baada ya kutokea ajali ya daladala na treni ya Pugu saa 11 leo alfajr makutano ya Nkrumah. Majeruhi wako 23.

Polisi Reli wanasema majeruhi wako 23 , Amana 8 na 15 wako Muhimbili. Kati yao watatu ni mahututi! Daladala lilikuwa kutokea Gongolamboto !

UPDATE:

Majeruhi 7 wapo Amana baada ya mmoja kuhamishiwa Moi! Jumla wahanga16 wapo Moi!

Chanzo cha habari ni TRL
 
Daladala lilikuwa linatoka Gongolamboto na Train linakwenda Pugu, hii inaonyesha ni wapinzsni wa jadi. Inawezekana daladala lilichomekea na kumuwekea bodi dereva wa Train
 
Watu 25 wamejeruhiwa na mmoja kufariki baada ya daladala kugonga treni katika eneo la Gerezani, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Hizi ni taarifa za awali, tutaendelea kukuhabarisha zaidi

Chanzo: ITV

Waliopo eneo la tukio watuhabarishe zaidi

UPDATE:

Majeruhi 7 wapo Amana baada ya mmoja kuhamishiwa Moi! Jumla wahanga16 wapo Moi
 
Nimesikia redioni kuwa mwenye daladala baada ya kuona gari za mbele yake zimesima ili tren ipite yeye akaovertak ili awahi ndo akapigwa na tren naishauri serikali kuwapima akili kwanza madeleva kabla ya kuwapa leseni
 
Kuna taarifa kuwa kuna daladala moja limeigonga treni maeneo ya karibu na kamati na kuna taarifa mtu mmoja kapoteza maisha!source...Clouds
 
Dereva wa daladala ni kwamba hajui alama za barabarani au ni katika harakati za kuwahi au kujitoa ufahamu??
 
Poleni sana waathiriwa wote wa mkasa huo wa ajali.. Na majeruhi mungu awape nafuu..!
 
Dereva wa daladala ni kwamba hajui alama za barabarani au ni katika harakati za kuwahi au kujitoa ufahamu??
inasemekana dereva wa daladala alikuwa anashindana na mwezake bahati mbaya mwenzake akapita yeye nae akasema tawahi matokeo yake ndiyo ajali.
 
Back
Top Bottom