Bado suluhisho ni kuhamia Dodoma, ila serikali haitahamia, hata Bunge lililazimika kwa vile walikuwa hawaenei Karimjee Hall, la sivyo ungewakuta bado wapo DSM. Ni kweli kuwa mji unatakiwa upanuliwe kutoka Bagamoyo hadi Utete, kuwe na Urban Railway halafu wajenge Administrative District kwaajili ya Serikali ya Muungano, karibuni tutakuwa na Serikali ya Tanganyika nayo itahitaji wizara etc. Kazi ipo. Yanayohitajika ni:
1. Urban Railway (Bagamoyo, Utete, Chalinze)
2. Maji ya kutosha kutoka mto rufiji.
3. Umeme wa kutosha.