Dar es Salaam biashara zinakufa kwa kasi sana

Dar es Salaam inachakaa kwa kasi ya ajabu. Mtaa wa Samora, moja ya mitaa ya jiji iliyokuwa kitovu cha biashara ya bidhaa halisi kwa sasa inatia huruma. Biashara ni kama hakuna na zilizobaki hazina wateja. Ule ukijani na marashi ya Mtaa wa Samora sasa ni historia.

Mabenki kama NBC ukienda pale Corporate Branch unakuta wateja kwa idadi ya single digit na tellers wawili tu ndo wako on duty. Dar es Salaam inakufa kwa kasi.

Nenda Mlimani City kuna fremu nyingi tu ziko wazi.

Pita eneo la viwanda Nyerere Road vitega uchumi vya Quality Group sasa hivi ni uwekezaji wa popo na jamii zingine za ndege wa usiku.

Kama nchi nadhani kuna shida mahala.

Rais ajae ana mtihani.
Zamani kupata fromu Kariakoo ilikuwa mtihani... leo hii eti siyo ISHU kubwa kisa watu wamefunga biashara... Samira Avenue Dar, eti like jengo opposite na Jengo la NHC next to extelecom house eti kuna vyumba vipo wazi..!!! Samora hii hii..!!
 
Dodoma ndiyo habari ya mjini
Nenda dodoma
Mimi nipo rukwa
Kwamba unaweza kushawishi watu wa Congo DR, Malawi, Zambia, Burundi waende Dodoma wakafunge mzigo?
Dodoma hakuna biashara yoyote kubwa ambayo Mbeya au Mwanza au Arusha hazipo. Mtoa mada anajaribu kuangalia biashara kwenye jiji kuu la Kibiashara
 
Hivi Kenya na Tzn nani ana rasilimali nyingi? Ukipata jibu jiulize kwa nini Kenya inaizidi Tzn maendeleo,ukipata jibu ndio hilo hilo linafanya mikoa yenye rasilimali nyingi kuzidiwa na Dom

Afu lengo la serikali sio kuifanya Dodoma iizidi Dar bali ni kufungua fursa nyingine ya biashara

Hata hivyo Dodoma ni Mji wa biashara given her geographical proximity ya kuwa katikati ya Miji mikuu
Dodoma ni mji wa biashara?
Mmmh, sina uhakika. Ni baishara za kawaida tu za vyakula na labda vifaa vya Ujenzi kwa kuwa makazi ya kuishi yanajengwa kwa wingi kwa sasa,lakini siyo biashara kubwa kwa muktadha wa biashara
 
Tatizo watu hatutaki kubadiri namna ya kufikiri. Watu tulio wengi tunaishia kulalamika tu lakini hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa kwa kulalamika. Wewe unapolalamika mwenzio anautumia ubongo vizuri anafanikiwa. Tazama watu wanaofanikiwa acha kuvutwa na wanaoshindwa. Kumbuka pia duniani nyakati zinabadilika. Kama Leo wazungu wasingefikiri wangeishije wakati walitegemea kutawala watu wengine ili inchi zao zikue kiuchumi.
 
Nilienda Acb main branch hakuna foleni nilishangaa sana..
Tellers wanachati tu
Nilikuwa na Dilham,Benki zote hole,mpaka kibanda cha posta ndo nikapona,wamachinga wa posta wote wamenuna,lazima tumemkosea mungu kwa kuingia uchumi wakati wakati pato la familia ni chini ya 1080
 
Dodoma ni mji wa biashara?
Mmmh, sina uhakika. Ni baishara za kawaida tu za vyakula na labda vifaa vya Ujenzi kwa kuwa makazi ya kuishi yanajengwa kwa wingi kwa sasa,lakini siyo biashara kubwa kwa muktadha wa biashara
Dodoma yenyewe ukifika CBE uko Mjini ukifika mwisho wa Airport kuelekea singida umemaliza mji,tunapigwa hakuna fact katika vitabu vya takwimu
 
Jamani tatizo syo Dar peke yake. Njoo hapa Arusha panatisha. Juzi nilikuwa Bagamoyo Pwani, kisha nikaenda Morogoro hali ni tete mno.

Huyu mponya korona anaharibu biashara na uchumi wa nchi.
Hatimae yametimia na hali bado ni tete
 
Wafanyabiashara wapo kwenye state ya Hibernation, wakisuburi mi-five again ipite. Ingawa kuna ka upepo ka ushirikina ka kiufanya hii mi-five again iwe again.
Serikali ilivyoondoa annual leave allowance,seminars na incentive Hapo wamefuta mrija wa oxygen katika mwili
 
Kuhusu Mabanki watu wanatoa pesa na kuweka kwenye simu sio lazima waende Bank ndio sababu foleni zimepungua ktk Mabenki yetu. pia ATM pia zimepunguza Msongamano Mkubwa. kibiashara kweli hali ni ngumu sana kwa nje na ndani covid 19 imechangia wageni kutosafiri kuja tanzania wakiogopa corona kumbuka nchi jirani ndio wadau wetu wakubwa ktka biashara.malawi,zambia , zimbabwe, na msumbiji, congo, burundi, rwanda , na uganda, na ndugu zetu wakenya , baharini kuna ndugu zetu wacomoro
 
Back
Top Bottom