'siku nzi akiacha ujinga anaweza kutengeneza asali'
kuna kampuni muundaji mzuri wa boti na meli. nadhani linaitwa Songoro kama sikosei. aisee kumbe tunaweza, sema tu ufahamu wetu tumeumbiwa kuthamini vya nje.
heko wazalendo, soon tutaendesha na magari ya kifaru toka lile kampuni letu kama litafufuliwa.
kuna haja mamlaka za ubora, costech kutupia jicho kwa wagunduzi na mafundi wenye nia ili waisogeze Tz katika aina nyingine ya uchumi kwa kupunguza mlolongo wa vikwazo na masharti.
yaani wagunduzi wajengewe uwezo+mitaji na wapewe kila msaada unaohitajika kutimiza ndoto zao kisha kazi (vilivyokamilika) wapewe wengine kuendeleza mchakato wa ubora, leseni, vibali na kusaka masoko. tumepoteza mawazo mengi kwenye ugunduzi wa helikopta, meli, magari, ndege/drones kwa wagunduzi kukosa vigezo vya mamla ikiwemo kubwa la mitaji.
cc. VETA
cc. SIDO