Dar city centre needs rearrangement | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar city centre needs rearrangement

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Danniair, Sep 3, 2012.

 1. D

  Danniair JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  If you walk along the Dsm city centre a.k.a Posta utakubaliana na mimi kuwa mji wetu ambao ilipangwa vizuri sana na Wajerumani kwa sasa mitaa yake haipendezi tena kama ilivyokuwa kabla ya ujenzi wa majengo ya kisasa.

  Wajenzi wa majengo ya kisasa wanaondoa kabisa maegesho ya wazi, wanajijengea uzio wanawanyima wa-tz haki ya kuegesha ktk maegesho ya wazi. La ajabu jiji wapo, wabia wao - NHC wanaowapatia viwanja wapo na mbaya zaidi hata nyumba zao hizo wanazopandisha juu hazina maegesho pia!!!!

  Rais alipowapa go ahead ya ubia hakumaanisha kuwa tuyaondoe maegesho ya wazi. Angalia picha za mitaa ktk miji mbali mbali ujionee mitaa inavyopendeza kwa maegesho ya wazi., lakini si hapa DSM.

  Tunao wenyeviti wa serikali za mitaa humu posta lakini hawathaminiwi wala kushirikishwa kabisa ktk majenzi yao. Je, kama ngazi ya chini kabisa haikushirikishwa itakuwaje waziri aliweze jambo hili? Mapato ya jiji yatokanayo na maegesho ya wazi yanayovunjwa na wajenzi hawa yanafidiwaje?

  Angalia pale mbele ya Tanzanite Suite (Morogoro road) huwezi hata kuthubutu kuegesha gari lako. Unafukuzwa kama mwizi. Aggrey street(pembeni mwa Golden Plaza), eneo kubwa kabisa la kutosha magari 2 hadi 3 limegeuzwa sehemu ya jengo. Mbele ya Avon na Niko Hotel parking pale si za watu wengine tena. Mbele ya jengo jeupe linaloangalia bustani India/Mosque streets utapenda!! sasa tembelea usiku ujionee utitiri wa magari yasiokuwa na pakingi.
  Kuwa na gari posta sasa imekuwa ni sawa na kuwa na mzigo usiobebeka.

  Ombi:mamlaka husika ikiwemo NHC wenye dhamana ya mitaa ya posta tufanyieni street rearrangment, sehemu za kubomolewa zibomolewe ili kuiweka mitaa yetu sawa. Wenyeviti wetu wasiache nyuma. Meya Jerry Slaa amka kama ulivyokuwa umeanza kuamka baada ya kuchaguliwa kwako. You are so smart by looking at you but the city you are leading is not well arranged like uncombed hair
   
 2. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,855
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Tatizo sio maegesho Tu Ila no defined pedestrian Routes!! Ukipita barabara ya Uhuru wenye Maduka wamepanga Bidhaa kunako Pedestrian way!! Hivi Kweli Hawa watu wanalipia Kodi Hiyo road reserve kwa waenda Kwa Miguu!! Hebu Aje hiyo Meya wa Ilala atufafanulie!!
   
 3. D

  Danniair JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asnte umeliona hilo. Hivi tuambiwe zile pakingi charges zinaenda wapi?
   
 4. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135

  Umeandika vizuri sana, mimi nafikiri tatizo lipo katika mfumo wa uongozi katika nchi yetu, kwa maana huwa najiuliza hivi mwenye mamlaka hapa ktk mji wetu ni nani?
  Je ni Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, au Meya? na hapo katika Meya wapo 4, kuna wa kila Wilaya halafu kuna wa Mji mzima (kama sijakosea), sasa ni yupi anawajibika wapi?
  kwa mfano hayo matatizo uliyoyaorodhesha yako chini ya nani?

  Hapo hapo kuna wizara ya Ardhi bila kusahau Tanroads na wote hao utasikia wameongea au kutoa maamuzi katika mambo mbali mbali kuhusu mji wetu!

  Halafu kingine, ni kwamba kuna siku Mkuu wa kikosi cha zima moto alikuwa anahojiwa, akasema sheria inasema kwamba, kabla ya jengo lolote kujengwa Dar ni lazima wao waidhinishe (Zima moto), na akasema uwezo wao wa kuzima moto Tanzania ni mwisho Ghorofa 8, kwa maana hiyo majengo yote yaliyo zaidi ya Ghorofa nane hawana uwezo wa kuzima moto na hivyo kwa maana nyingine yote hayo hayakupaswa kujengwa kwa maana hayakupata kibali, lakini cha kushangaza zaidi majengo karibu yote marefu ni ya Taasisi za Serikali kwa maana hiyo wao ndio vinara wa kuvunja Sheria za nchi!
   
Loading...