Fahari ya kusini
JF-Expert Member
- Nov 26, 2022
- 427
- 1,668
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemuhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa, Abel Stephano baada ya kumkuta na hatia ya kumuua mkewe Nuru Karim, kwa kumnyonga na kamba ya viatu.
Licha ya Abel kukana mahakamani kutenda kosa hilo, alikiri kuwa yeye na mkewe (marehemu) walikuwa na ugomvi mdogo katika ndoa yake kwani alitaka mkewe abadilishe dini na kuwa Mkristo lakini mkewe hakukubali.
Upande wa mashitaka ulieleza Mahakama kuwa tukio hilo lilitokea Julai 24, 2023 wakiwa nyumbani kwao eneo la Kitunda Mzinga ambapo wakiwa chumbani ugomvi baina yao ulitokea (Nuru) akitaka kwenda kwao.
Ilielezwa kuwa Abel alikutwa chumbani kwao huku mkewe marehemu akiwa amefariki dunia akiwa amelala kitandani na chini ya kitanda hicho kulikuwa na kamba ya kiatu iliyoelezwa kutumika kumnyongea hadi kufa.
Kwa mujibu wa upande wa mashitaka, mshtakiwa alifanya hivyo ikiwa ni njia ya kumzuia marehemu asitoke nje ya nyumba hiyo na baada ya kutekeleza kitendo hicho alipiga kelele kuomba msaada, kwani hakuwa na funguo za mndani, tukio liliripotiwa kwa mwenyekiti wa mtaa huo ambaye pia alitoa taarifa polisi na Abel kupelekwa Kituo cha Polisi cha Stakishari