Dangote yafafanua kusimama kwa shughuli za uzalishaji

View attachment 441429View attachment 441430Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limekanusha madai ya kuhusishwa na kile kinachotajwa kuwa ni sababu ya Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara kupata hasara na hata uzalishaji Kuzorota

Tamko hili linakuja siku moja baada ya kiwanda cha Saruji cha Dangote kutoa taarifa ikieleza uzalishaji umesitishwa kutokana na hitilafu ya mitambo huku pia suala la uzalishaji kwa kutumia Majenereta ya dizeli yakitajwa kukwamishwa shughuli hiyo

Kupata ufafanuzi zaidi hii leo katika Azam News watakuwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Chanzo : Azam News

TPDC hawana ubunifu wowote,kwa miaka mingi wapo tu wanaenda mafunzo nje ya nchi,na kulipana posho za usd! lazima wabadilike waanze kussupport wawekezaji km hawama imagine plant ya 600USDmio inazimwa kisa input za production hamna! why tra wasiwaruhusu dangote wa import mafuta yao via BPS wayatumie baada kulipa duties nk,kwa nini waende wakanunua kwenye OMC ambazo zinaweka cost zao+margin ambazo inakua mzigo kwa wawekezaji!
kwa nini serikali isianze kuaondoa kodi kwy mafuta yanayotumika kwy uzalishaji wa cement km walivyofanya kwy baadhi ya migodi??
TPDC wajipange la sivyo watumbuliwe tu hamna namna.
 
View attachment 441429View attachment 441430Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limekanusha madai ya kuhusishwa na kile kinachotajwa kuwa ni sababu ya Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara kupata hasara na hata uzalishaji Kuzorota

Tamko hili linakuja siku moja baada ya kiwanda cha Saruji cha Dangote kutoa taarifa ikieleza uzalishaji umesitishwa kutokana na hitilafu ya mitambo huku pia suala la uzalishaji kwa kutumia Majenereta ya dizeli yakitajwa kukwamishwa shughuli hiyo

Kupata ufafanuzi zaidi hii leo katika Azam News watakuwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Chanzo : Azam News
Taarifa ya Dangote cement ilitufikia kupitia mitandao ilikuwa na jina na sahihi ya mkurugenzi wa Dangotw cement. unatuambia tuipuuze maanake ni feki? Au haina lalamiko lenye maana?
Hii taarifa ya TPDC imetufikia kupitia mitandao, haina mhuri, haina jina la afisa aliyeandika wala sahihi. Vipi tuipuuze? Au tuamini kuwa imetoka kwenye genuine source?
 
Hili suala la Dangote kusitisha uzalishaji wa saruji kwa Mikoa ya Kusini inabidi Serikali ilifanyie kazi na kupata suluhisho. Vinginevyo sumu itakayomwagwa na wapinzani itafanya CCM kuchukiwa sana hasa Mikoa ya Kusini. Dangote amekuwa mkombozi kwa Mikoa ya Kusini.Leo hii mfuko wa saruji inauzwa shs17,000 badala ya 10,000 kule Mikoa ya Kusini.
 
TPDC wamejichanganya,Dangote hawajasema kuhusu kunyimwa gesi,bali ni habari zilizoenezwa na watu wasioitakia mema Tanzania ya viwanda,siku nyingine TPDC kuweni makini katika kujibu.
 
Taarifa ya Dangote cement ilitufikia kupitia mitandao ilikuwa na jina na sahihi ya mkurugenzi wa Dangotw cement. unatuambia tuipuuze maanake ni feki? Au haina lalamiko lenye maana?
Hii taarifa ya TPDC imetufikia kupitia mitandao, haina mhuri, haina jina la afisa aliyeandika wala sahihi. Vipi tuipuuze? Au tuamini kuwa imetoka kwenye genuine source?
1480521611451.jpg
Kama ni muhuri au sahihi hii hapa.... Kaimu mkurugenzi wa Shirika la maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Mhandisi Kapulya Musomba akakanusha madai ya Dangote
 
Serikali,kupitia kwa Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe. Charles Mwijage,imetoa ufafanuzi kuhusu kufungwa kwa kiwanda cha Dangote cha kuzalisha saruji huko Mtwara.

Waziri Mwijage amesema kuwa Dangote wamefunga kiwanda chao kupisha ukarabati wa mitambo yao kiwandani humo na si vinginevyo. Wakati huo huo,Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, amesema kuwa hakuna mgogoro wowote uhusuo uagizwaji au upatikanaji wa makaa ya mawe kwa viwanda hapa nchini.

Chanzo: ITV Habari
 
Kwa msemo wa waswahili wanafunika kombe, mwanaharamu apite!
 
Vituko sasa hivi, tangia lini serikali imekuwa msemaji wa viwanda binafsi.

Okay, kesho wakumbue kutuletea taarifa ya Sao Hill pia.
 
member: 390326"]DK. KAFUMU on DANGOTE (A must read).

"Hii ni shida yetu watanzania wote, wataalamu, viongozi wa serikali na pia wanasiasa. Kwanza tuko SLOW, sijui tunaogopa kutoa maamuzi? Sijui ni taaluma duni? Sijui ni nini? Mwekezaji DANGOTE, tuliahidi kumpa malighafi ya LIMESTONE kwa ajili ya kuzalisha SARUJI kwa unafuu mkubwa; tuliahidi kumpa ardhi kwa bei nafuu au bure; tuliahidi kumpa gesi nyingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa makaa ya mawe kwa wingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa nafuu ya kodi na mengine mengi; mazingira yaliwavutia (Dangote na wenzake) sana. Dangote wakavutika wakaja. Mimi (Dk. Kafumu) nikiwa Kamishna wa Madini wakati huo nilitimiza wajibu wangu wa kuwapa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa LIMESTONE kadri ilivyohitajika. Nawashukuru sana STAMICO walinisikiliza na kiwanda kijajengwa. Awamu ya tano (ya JPM) imekuja na mambo mapya, ahadi zingine (kwa wawekezaji) zinasuasua, sijui ni nini! Prof Mjebda (anamtaja Prof. mwingine kwenye Whatsup Group) anaweza kutuelimisha hapa. Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa ikiwa ni pamoja na nchi kupata kodi za kutosha; ajira zitapatikana; sekta ya majenzi (ujenzi) itaimarika; uchumi utaimarika. Ni muhimu tuwahamasishe (wawekezaji) tuangalie matokeo ya muda mrefu na siyo haya ya haraka. Kiwanda kikifungwa shida ni yetu, hebu tuwe na mioyo ya kibiashara siyo siasa za uzalendo uchwara. Samahani sana "

Dkt. Dalali Kafumu,
Kamishna Mstaafu wa Madini (Tanzania),
Mbunge wa Igunga (wa sasa),
Kada wa CCM.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]; Nimehariri lugha kwenye maoni hayo ya kitaalamu ya Dk. Kafumu. Tujadili seriously.
JSM.[/QUOTE]Kafumu anasema haya
 
Serikali,kupitia kwa Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe. Charles Mwijage,imetoa ufafanuzi kuhusu kufungwa kwa kiwanda cha Dangote cha kuzalisha saruji huko Mtwara.

Waziri Mwijage amesema kuwa Dangote wamefunga kiwanda chao kupisha ukarabati wa mitambo yao kiwandani humo na si vinginevyo. Wakati huo huo,Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, amesema kuwa hakuna mgogoro wowote uhusuo uagizwaji au upatikanaji wa makaa ya mawe kwa viwanda hapa nchini.

Chanzo: ITV Habari
Kuna viwanda kama TBL sijasikia eti wamefunga kiwanda kufanya marekebisho. Inamaana viwanda vya wengine huwa hawafanyi repair.
 
TPDC wamejichanganya,Dangote hawajasema kuhusu kunyimwa gesi,bali ni habari zilizoenezwa na watu wasioitakia mema Tanzania ya viwanda,siku nyingine TPDC kuweni makini katika kujibu.
Nilichofurahishwa ni kuwa Waziri mwenye dhamana, kajitokeza kwa kasi ya mwanga mbele ya kioo kuzikanushilia mbali zao za kizushizushi, cjui wanazipataga wapi tu!
Kiwanda kufanyiwa "service" tafsiri yake ni kufunga biashara na uzalishaji?
 
Back
Top Bottom